Rais William Ruto amesema kwamba hatakubali “kutoijali nchi” baada ya maandamano ya ghasia kukumba mji mkuu, Nairobi na mji wa magharibi wa Kisumu.

Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanasiasa wa upinzani Raila Odinga ambaye analaumu sera za serikali kwa kuzidisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Pia amedai bila ushahidi kwamba alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

“Nitahakikisha kama rais kwamba nchi hii inaongozwa na sheria, na hakuna chochote zaidi ya sheria na katiba kitakachokuwa sehemu ya kile tunachofanya,” Bw Ruto alisema.