Na Helena Magabe , JamhuriMedia, Tarime

Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda ameishauri Halmashauri ya Tarime vijijini kutumia mapato ya ndani kumalizia miradi viporo ili ikamilike na kutumika.

Hayo ameyasema hayo Juni 21,2023 katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika kwenye ukumbi wa JK Nyerere Nyamwaga.

Mtanda amesema madiwani wanatakiwa kusimamia miradi ya maendeleo ambayo ni viporo kwa sababu Halmashauri hiyo inakuzanya zaidi ya shilingi bilion 8 lakini hata fedha zinapokuja zinachelewa kutumika.

” Fedha zinakuja zinakaa miezi mitatu mhandisi,afisa manunuzi pamoja na engineer hawa watu watatu huwa wanannisumbua sana wanachelewesha miradi unatakiwa ufanyike ukaguzi mzuri wa miradi kwani muathirika wa Kwanza ni mwananchi wa pili Chama na wa tatu Diwani” amesema Mtanda.

Akiendelea kuzungumza amesema miradi magofu ikamilike ili wananchi wahudumiwe kwa wakati kwa sababu inapokea fedha za CSR bilioni 7.5 ambazo zinatakiwa ambapo alimhakikishia zikamilishe miradi watu wahudumiwe vizuri na kwa wakati.

Amesisitiza mbunge wa Tarime Vijijini kutolia tena Bungeni kwani anataka fedha ya CSR iletwe kwenye baraza ijadiliwe kwa nini Kuna changamoto ya ucheleweshwaji wa fedha hiyo hali inayokwamisha miradi kutekelezeka kwa wakati kwa sababu fedha hiyo sio ya hisani bali ni wajibu itolewe.

Amefafanua kuwa kila mwaka fedha hiyo ingetekeleza miradi ya kimkakati kwa mwaka mradi wa bilioni 1 mwaka mwingine mradi wa bilioni 2 na mwaka mwingine mradi wa bilioni 3 fedha zinazokuwa zimebakia baada ya mradi kukamilika wanashare kwenye maendeleo mengine isiwe ni siasa zaidi kuliko uharisia.

Akiendelea kusisitiza juu ya fedha za CSR amesema watakaa kikao na Madiwani na menejimenti ya mgodi lakini hawataingilia fedha hizo na badara yake wanataka kujua changamoto ya ucheleweshwaji na zinapoingia zifanye miradi yakinifu.

Aidha ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kwa miaka sita mfurulizo ambapo Halmashauri imekusanya bilion 8 Marengo yalikuwa bilion 7 sawa na asilimia 110.

Ameipongeza kuwa Mkoa wa Mara hautakiwi kuwa wa mwisho kwa mapato unatakiwa kukua usemwe kwa mazuri iondolewe taswira mbaya wawekezaji waje kwani Mkoa usio na wageni hauwezi kuendelea.

Katika hatua nyingine Halmashauri ya mji Tarime nao wamepata hati safi kwa mfurulizo wa miaka mitatu.

Halmashauri hiyo imeshauliwa isiibue miradi kisiasa waepuke makundi kwani yeye hana makundi na hatabadirika ambapo amewataka kurudisha shilingi milioni 560 ya mkopo kwa ajiri ya upimaji viwanja inatakiwa irudishwe mwisho tarehe 15/7/2023 ni lazima alimtaja afisa Ardhi kusababisha changamoto za migogoro ya ardhi.

Amesema Rais Mama Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi lakini usimamizi unakuwa dhaifu na kuongeza kuwa fedha za mapato ya ndani zikamilishe miradi viporo zisiibue miradi ya kisiasa.

Hata hivyo Halmashauri hiyo impokea zaidi shilingi bilion 9.1 kwajili ya miradi mbali mbali na kwa kupitia mapato ya ndani imejenga shule mbili na zahanati moja.

Aidha Halmashauri hiyo ina kilio cha muda mrefu juu ya mkandarasi ambaye amegoma kurejesha vibanda 9 vya maduka baada ya Halmashauri kuchangia ujenzi shilingi milioni 48.

Makubaliano yalikuwa baada ya ujenzi kukamilika Halmashauri imiliki vibanda hivyo kwa kukusanya kodi ya pango lakini baada ya kuisha mambo yalibadirika mkandarasi ndiye anakusanya kodi na kulipa ushuru tu Halmashauri hiyo.

Hata baada ya kikao kuisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Daniel Komote ameahidi kushirikiana na Mkuu wa Mkoa na kuwataka waandishi waandike kuwa halmashauri hiyo imepata hati safi.

Komote amewataja kwa majina na wengine kwa vyombo vyao huku wakisimama kitendo ambacho si sahihi kwa tasnia ya habari kwani kinachangia kuwagawa waandishi wa habari

By Jamhuri