Watatu kuunganishwa na Badwel?
Wakati Badwel akiwa tayari keshapandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaa , JAMHURI imedokezwa kwamba kuna wabunge wengine watatu wanaokabiliwa na hatihati ya kuunganishwa pamoja na mtuhumiwa huyo.

Imeelezwa kwamba wabunge hao wanne akiwamo Badwel, ndiyo waliosuka mpango wa kuomba rushwa kutoka kwa Mkurugenzi huyo wa Mkuranga. Baada ya makubaliano, Badwel ndiye aliyetumwa kuzipokea fedha hizo na akaishia kunaswa katika mtego maalumu uliowekwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

By Jamhuri