Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Prof.Joyce Ndalichako, amesema serikali imeendelea kuwapatia mafunzo ya uzoefu kazini vijana ikiwamo wanaohitimu masomo yao nje ya nchi.

Amesema Ofisi hiyo kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira (TAESA) kimekuwa kikiratibu utoaji wa mafunzo ya uzoefu kazini kwa vijana wakati wakisubiri ajira.

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Aprili 24, 2023 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum, Fakharia Shomar Khamis aliyehoji serikali inawatengenezea mazingira gani vijana waliofadhiliwa masomo nje ya nchi pindi wanapohitimu ili waishi maisha bora.

Akijibu swali hilo, Mhe. Waziri Ndalichako amelihakikishia Bunge kuwa Serikali imeendelea kutoa ajira kupitia sekretarieti ya ajira na sekta binafsi ambayo inakua kwa kasi kubwa huku ikitengeneza mazingira ya kuwapatia mafunzo ya uzoefu kazini.

By Jamhuri