N Mwandishi Wetu, Jamhuriamedia, Dar ea Salaam

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amepongeza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada mbalimbali za kurejesha hali katika maeneo ambayo miundo mbinu ya barabara imeathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake leo tarehe 21/01/2024 Mkoani humo alipotemebelea na kujionea athari za mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia tarehe 20/ januari/2024 na kuathiri maeneo mabalimbali ya wilaya ya Kindondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Jiji la Ilala.

Naibu Waziri Ummy amesema anampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abert Chalamila kwa uongozi ambao wameuonesha katika kurejesha halina kazi waliyofanya.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Uratibu Mhe. Ummy Nderianga alipotembelea kuona maungio ya daraja la Kunduchi barabara ya Kunduchi yalioathirika kutokana na mvua za vuli zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Saalam.

“Naomba tufanye kazi hii usiku na mchana ili tuweze kurejesha hali mapema bila kuathiri shughuli za biashara na shughuli nyingine za uchumi zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es saalam,” alihimiza.

Sisi kama Serikali tunawahakikishia wana Dar es salamu kwamba tutafanya kazi hii ya urejeshaji wa hali kwa nguvu bila kuchoka,
Naye Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Saad Mtambule amesema kazi waliyofanya ni kusimamia usafishaji wa mitaro na usawishaji wa mito na hivyo kusaidia maji kutotuwama kwa muda mrefu.

“Tumeendelea kuwaeleza wananchi walio katika maeneo ya pembezoni mwa mito kama; Mto Nyakasangwa, Mto Mpiji, Mto Tegeta, Mto Mlalakuwa na Mto Ng’ombe kuhamia maeneo ya juu ili kuepeuka athari za mvua,”alibainisha.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Uratibu Mhe. Ummy Nderianga akielekeza jambo kwa mratibu wa maafa mkoa wa Dar es salaam Bw, Gerad Sondo wakati alipotembelea kujionea juhudi za urejeshaji hali katika maungio ya Daraja la Mbopo barabara ya Madale katika jiji la Dar es salaam.

Ujenzi wa nyumba holela umesababisha Watu kujenga mpaka kwenye mapito asili ya maji na kusababisha maji kukosa sehemu za kupita na kuingia maeneo ya watu.

“Lakini pia tuna kazi ya kuendelea kuwaelimisha wananchi ili wafuate misingi ya ujenzi wa maeneo kulingana na ramani ya mipango Miji,” amesisitiza.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderianga akizungumza na wananchi (hawapo katikapicha) wakati alipotembelea kuona urejeshaji wa maungio ya daraja katika ya barabara ya Tanganyika katika daraja la Mbweni yaliyoathiriwa kutokana na Mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkazi wa Ununio Bw. James Koyi ameishukuru serikali kwa kazi kubwa inayofanya ya urejeshajji wa hali katika maeneo yaliyoathirika mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Dar es salaam.

Hakuna aliyejua kama mvua itanyesha masaa ishirini na nne hata hivyo serikali iendelee kufanya kazi katika kurejesha hali, alisema.

Katika picha ni baadhi ya maungio ya madaraja ambayo yameathrirka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na juhudi kubwa zikifanywa na serikali usiku na mchana katika kurejesha mawasiliano ya barabara katika maeneo ya maungio ya madaraja hayo ili yaendelee kupitika
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderianga akiwa amembeba mtoto wakati alipotembelea kuona urejeshaji wa maungio ya daraja katika ya barabara ya Tanganyika katika daraja la Mbweni yaliyoathiriwa kutokana na Mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.