BAO pekee la kiungo Jonas Mkude dakika ya 86 lililoipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Simba SC imefikisha pointi 10 baada ya ushindi huo na kuungana kileleni na mabingwa watetezi, Yanga kwa kulingana hadi wastani wa mabao baada ya wote kucheza mechi nne.

By Jamhuri