Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amesema ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi , Mashirika ya Umma na Wadau wa michezo.

Amesema hayo leo Septemba 16, Bungeni jijini Dodoma,wakati akijibu swali wa Shaban Omari Shekilindi (Lushoto) aliyeuliza Je ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo katika Mji wa Lushoto.

Napenda kutumia nafasi hii, kuzikumbusha Halmashauri nchini ikiwemo Halmashauri ya Lushoto, kuzingatia matakwa ya Sera ya Michezo kwa kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu ya michezo” amesema Gekul.

Gekul ameeleza kuwa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 ibara 7 inaeleza jukumu la ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la watu wote na mazingira ya kuwekeza yameainishwa kwa uwazi

By Jamhuri