Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imeanza uchunguzi wa miradi 79 yenye thamani ya sh Bil 34.5 iliyobainika kuwa na mapungufu katika sekta mbalimbali sambamba na uliyokuwa na mapungufu wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.

Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU mkoani humo Frank Mapunda amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024.

Amesema kuwa miongoni mwa miradi hiyo miradi minne imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yaliyopelekea kuanzisha kwa uchunguzi ambapo ameitaja hiyo kuwa ipo katika sekta za Elimu, Barabara, Maji na Afya.