Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dar

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), kimesema kuwa wafayakazi watulie kuhusiana na tozo za miamala ya benki kwani wamefikisha maombi serikalini kufanya mabadiliko ya sheria ya tozo ili kuepuka malipo ya mara mbili kwenye mshahara wa mtumishi wa umma.

Hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Kimataifa TALGWU, Shani Kibwasali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 huku Chama kikiwa na mafanikio ya kiutendaji katika kuangalia maslahi ya wafanyakazi.

Shani amesema tozo za mara mbili kwa mfanyakazi ni mzigo kutokana na mishahara yao kuwa midogo ambao haukidhi mahitaji ya kila siku na familia zao.

Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Kimataifa-TALGWU Shani Kibwasali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 huku Chama kikiwa na mafanikio ya kiutendaji katika kuangalia maslahi ya wafanyakazi.

Amesema tozo za kibenki lililoanza kutekelezwa hivi karibuni zinawaathiri sana wanachama wetu kwa kila mwezi wanalipa Kodi kwa kukatwa katika mishahara yao.

“Lakini sasa kuanza kuanza kutekelezwa kwa tozo ya Serikali kwa miamala ya kutoa na kuhamisha fedha katika benki inamfanya mtumishi wa umma kutozwa zaidi ya mara mbili katika kipato moja kwa mwezi, ambacho hicho hicho kinachokatwa ni kidogo”.amesema Shani

Aidha amezungumzia suala la nyongeza ya mishahara a kubainisha kuwa wanachama wao ni wahanga wakubwa kwani bado kuna manung’uniko ya nyongeza hiyo ya mshahara.

“TALGWU kama msemaji wao hawajaridhika na nyongeza ya mshahara ilivyofanyika” amesema Shani.

“Naomba niwatoe hofu wanachama wetu kwamba suala hili linashughulikiwa na Chama kwa kushirikiana na shirikisho la vyama huru vya Wafanyakazi nchini (TUCTA),”amesema Shani

By Jamhuri