Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027.

Rais Samia amesema nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.

Aidha, Rais Samia amesema michuano hii itachangia katika ukuaji wa utalii kwa kuwa ni mashindano ambayo hutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja Barani Afrika na maeneo mengi duniani kwa ujumla.

Vilevile, Rais Samia amesema mashindano hayo yataleta watu mashuhuri nchini wenye ushawishi duniani hivyo huwezesha na kunufaisha sekta nyingi za uchumi ambapo huchangia ajira, mapato kwa wafanyabiashara na serikali.

Kwa upande mwingine Rais Samia amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imeshafanya utafiti na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Mashindano ya AFCON yataweka rekodi kwa mara ya kwanza kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 1957.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027, kutoka kwa Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Mei 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Fulana iliyokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo Mhe. Balozi Pindi Chana, wakati wa kukabidhi andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027, kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Mei 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Fulana iliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, wakati wa kukabidhi andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda

By Jamhuri