Na Mwandishi Wetu

Wadhamini wa ‘wajelajela’ Tanzania Prisons ya Mbeya, Silent Ocean, wametoa ahadi ya milioni 20 kwa wachezaji wa timu hiyo ikiwa watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Yanga SC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili tarehe 4 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Tanzania Prisons waliopo nafasi ya 11 wakiwa na point 15 baada ya kucheza mechi 14 ikiwa wataifunga Yanga watakuwa wametia chumvi kidonda kwa kuwafanya mabingwa hao wa kihistoria kuchezea vipigo viwili mfululizo baada ya kipigo cha kwanza cha 2-1 walichokipata siku ya jana toka kwa Ihefu SC ambayo imeikomesha rekodi ya Yanga ya kutofungwa mechi 49 mfululizo. 

Wajelajela hao hawataondoka mikono mitupu pia ikiwa watafanikiwa kupata sare dhidi ya Yanga  kwa kuwa mdhamini wao, Silent Ocean, amewawekea kitita cha milioni kumi kwa matokeo ya sare ya aina yeyote.