Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Tanzania imesainia Mkataba wa Ushirikiano na Nchi ya Hungary katika sekta ya maji ili kubadilishana uzoefu wa teknolojia katika sekta hiyo.

Akizungumza leo Machi 28,2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Janury Makamba amesema kwa miaka mingi nchi hiyo inaongoza kwa teknolojia ya juu Duniani katika udhibiti wa maji ikiwemo maji taka,mafuriko na ya kunywa hivyo ushirikiano huo wa karibu utaleta tija kubwa kwa Taifa .

Sambamba na hayo amesema nchi hizi mbili zimekuwa zikifanya biashara hivyo kutafanyika makongamano ya kibiashara, ziara ili fursa zilizopo zifahamike na ushirikiano huo uendelee kudumu siku hadi siku.

“Tanzania ina vivutio vingi vya utalii na Hungary ni chanzo cha watalii kwani tumeshuhudia watalii wengi kutoka nchi hiyo wakija kutalii na miaka iliyopita walikuwa 5000 mwaka jana wakifikia 11000 hivyo kuna ongezeko kubwa kutoka nchi hiyo na kwa kuona hilo tumezungumza kwa kina na kujubaliana kuwa tutasaini usafiri wa anga watalii na wafanyabiashara watatoka moja kwa moja kutoka Hungary kuja Tanzani kwa ndege”Amesema Makamba

Sanjari na hayo amebainisha kuwa Vijana wa kitanzania wamekuwa wakinufaika kwa kupata ufadhili wa kwenda kusoma Hungari pia wamekubalina kunzisha mahusiano ya kituo cha Diplomasi cha kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salimna na chuo cha Diplomasia ambapo itasaidia wanadiplomasia kupata fursa ya kwenda Hungari kuongeza ujuzi.

Waziri Makamba amesema nchi ya Hungary wamedhamiria kuwekeza kwenye kiwanda cha kuwekeza ndege ndogo pale Morogoro na

Aidha nchi ya Hungary imekubali kujenga Ubalozi wao nchi Tanzania uliofungwa miaka ya 1990″ hiyo ni moja ya kusaidia kuongeza mashirikiano makubwa baina ya nchi hizo mbili.

Naye Waziri wa Mambo ya nje na Biashara wa Hungary Mhe Peter Szijj’art’o amesema licha ya kufungwa kwa ubalozi lakini bado ushirikiano ikuwa unaendelea hivyo habari njema ni kuwa nchi yao mwaka huu Julay inatarajiwa kuchukua Urais wa Umoja wa Ulaya.

By Jamhuri