Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA

Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe amefariki dunia leo asubuhi Katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni Jijini DSM.

Taarifa za awali kutoka vyombo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa Membe alipata changamoto ya kifua na kupelekwa Hospitali Alfajiri ya leo na baadaye akafariki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia mitandao ya kijamii ameandika kupokea kwa masikitiko kifo cha Membe.

By Jamhuri