Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limesema makadirio ya watoto milioni 400 walio chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na manyanyaso majumbani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limesema makadirio ya watoto milioni 400 walio chini ya umri wa miaka mitano, ikiwa sawa asilimia 60 ya wototo wote wa umri huo duniani kote wanakabiliwa na adhabu ya kipigo au kisaikolojia majumbani mwao, zikiwemo kuchapwa viboko hadi kutukanwa.

Makadirio mapya ya UNICEF yanaonyesha data kutoka katika nchi 100 zilizokusanywa kuanzia 2010 hadi 2023, na inashughulikia adhabu ya kimwili na za kisaikolojia.

Kwa UNICEF, unyanyasaji wa kisaikolojia unaweza kujumuisha kumzomea mtoto, au kumwita “mpumbavu” au “mvivu,” wakati unyanyasaji wa kimwili ni pamoja na kumtikisa, kumpiga au hatua yoyote inayokusudiwa kusababisha maumivu ya kimwili au usumbufu hata pasipo kumsababishia maumivu.

Kwa mujibu wa UNICEF zaidi ya mama mmoja au mlezi anayewajibika kwa mtoto kati ya wanne anaamini kwamba adhabu za kimwili ni muhimu ili kuwasomesha ipasavyo watoto wao.