Ukraine imesema kwamba mashambulizi ya makombora ya Urusi yamewajeruhi watu kadhaa na kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo huku Urusi nayo imeripoti vifo vya watatu katika mji wake wa kusini wa Tula.
Ukraine na Urusi zimeendelea kushambuliana kwa makombora usiku wa kuamkia leo. Ukraine imesema kwamba mashambulizi ya makombora ya Urusi yamewajeruhi watu kadhaa na kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, Meya wa mji mkuu wa Kyiv, Vitali Klitschko amethibitisha mashambulizi hayo ambayo kwa sehemu kubwa yanatajwa kuulenga mji wake.
Kwa upande mwingine, Urusi nayo imeripoti vifo vya watatu katika mji wake wa kusini wa Tula kufuatia shambulio la droni la Ukraine.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema hapo jana kwamba atafanya mazungumzo kuhusu mashambulizi ya Urusi na juhudi za kuumaliza mzozo huo wakati wa mkutano wake na Rais Trump wa Marekani watakapokutana katika mkutano wa kilele wa G7 nchini Ufaransa unaoanza hii leo.



