Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuachiliwa kwa wafungwa wa kivita kama sehemu ya makubaliano kati ya Ukraine na Urusi.

Makubaliano hayo yalifanikisha kiasi cha wanajeshi 200 waliokuwa wakishikiliwa katika pande zote za mzozo kurejeshwa kwenye mataifa yao.

Rais Zelensky alisema mpango huo umefanikisha wanaume 80 na wanawake 20 kurejea Ukraine na miongoni mwao ni pamoja na waliopambania jiji la Mariupol na kiwanda cha chuma cha Azovstal, ambacho kipo chini ya udhibiti wa Moscow tangu miezi ya mwanzo ya vita.

Wizara ya Ulinzi Moscow imesema askari wake waliokuwa wakishikiliwa na Kyiv wameachiliwa baada ya mchakato wa mazungumzo.

Urusi na Ukraine mara kadhaa zimekuwa zikibadilishana wafungwa wa kivita tangu mwanzoni mwa uvamizi wa Moscow mnamo Februari 2022, ikiwa ni mfano wa nadra wa mawasiliano ya bayana baina ya mahasimu.

By Jamhuri