Ukraine imedai kushambulia na kuharibu madaraja na maghala ya silaha pamoja na kuviharibu kabisa vituo vya kuongoza shughuli za kijeshi katika eneo lililokuwa likidhibitiwa na Urusi la Kusini mwa Ukraine.

Urusi nayo imesema imelipiza shambulizi hilo la kuuwa wanajeshi kadhaa. Mapigano yametokea katika eneo la Kherson ambako wanajeshi wa Urusi walipata mafanikio makubwa ya kulidhibiti eneo hilo mwanzoni mwa vita nchini Ukraine.

Mashambulizi yaliyofanywa leo na wanajeshi wa Ukraine yamezidisha tetesi kuhusu opresheni yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya Urusi. Wizara ya ulinzi ya Uingereza kwenye ripoti yake ya kiintelijensia imesema wanajeshi wengi wa ukraine wameimarisha mashambulizi yao ya makombora katika eneo la kusini linalodhibitiwa na wanajeshi wa Urusi.

By Jamhuri