Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Dodoma Mjini Isack Ngongi amewataka vijana kuungana kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Ngongi ameyasema hayo leo Januari 15,2024 jijini hapa wakati akigawa vyeti wa wanafunzi wa Chuo ya Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na Chuo cha Madini waliohitimu mafunzo ya itifaki, usimamizi wa mikutano na uongozi.

Amesema hivi karibuni kutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa vijana tumejipanga na hatutakubali kupoteza mtaa hata mmoja.

“Kuna chaguzi ziko mbele yetu sisi kama vijana tunatakiwa kuungana kuwa kitu kimoja kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Tutahakikisha tunatafuta kura nyumba kwa nyumba ili kuendelea kushika dola ambapo ndio ndoto ya chama chochote cha siasa,” amesema.

Kuhusu vijana waliohitimu mafunzo hayo Ngogi amewasisitiza kuwa na heshima na kuwa mstari wa mbele kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia.

Adhia amewahamasha vijana kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha Mipango na Mujumbe wa Balaza la UVCCM Mkoa wa Dodoma Sebastiani Tarimo amesema wanafunzi 65 wamehitimu mafunzo hayo na kupewa vyeti.

Amesema mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili ambapo vijana hao walishiriki na sasa wapo tayari kutumika katika shughuli mbalimbali za chama na serikali.

Naye Muhitimu wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Mazingira (MISO) Amina Paschal amesema mafunzo hayo yalikuwa mazuri na yatasaidia katika kuongeza heshima na kupanua wigo wa kutumikia chama katika shughuli mbalimbali.