Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Sherehe za Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) tarehe 19 Machi, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na Wananchi wa Mikoa mbalimbali wakiwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda kabla ya kuhutubia Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi katika Sherehe za kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

By Jamhuri