Vanessa Mdee anatarajia kuachia albamu yake mpya mwakani chini ya Universal Music Group ambayo kwa sasa ndio wasimamizi wa kazi zake za muziki.

Vee Money amesema baada ya kusaini mkataba huo sasa yuko tayari kuachia albam katikati mwakani na kwamba kampuni hiyo itakuwa ikisimamia kazi zake katika bara la Ulaya na Afrika.

Muimbaji huyo amesema albamu hiyo itatoka mwezi wa sita mwakani chini ya kampuni ya Universal ambapo kwa mkataba wa aina yake ambao amesaini unamfanya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kupata dili nono kama hilo katika kampuni hiyo.

Msanii mwengine wa Bongo Flava ambaye anafanya kazi na kampuni ya Universal kutoka Tanzania ni Diamond Platnumz.

By Jamhuri