Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma
VIJANA nchini Tanzania wanaendelea kurasimisha shughuli zao za biashara kwa kasi, hali inayoashiria kuongezeka kwa ushiriki wao katika uchumi rasmi na mchango wao katika juhudi za maendeleo ya taifa.
Hayo yameelezwa leo Aprili 15,2026 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.Godfrey Nyaisa, wakati wa Semina kwa madiwani wa Halmashauri ya Dodoma .
Bw.Nyaisa amesema takwimu za BRELA zinaonesha kuwa maelfu ya kampuni, majina ya biashara na alama za biashara na huduma (trade and service marks) zilizosajiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita zinamilikiwa na vijana. Hali hii inaonesha wazi kuongezeka kwa mchango wa vijana katika sekta za viwanda na biashara nchini.
“Kampuni 5,045 zimesajiliwa, ambapo 3,120 zinamilikiwa na vijana. Aidha, majina ya biashara 8,792 yamesajiliwa, kati ya hayo 4,938 ni ya vijana. Kwa upande wa alama za biashara, jumla ya 1,018 zimesajiliwa, nyingi zikiwa zinamilikiwa na vijana. Vilevile, leseni za biashara daraja la “A” 5,430 zimetolewa, ambapo takribani nusu yake zimekwenda kwa vijana.”amesema Bw.Nyaisa
Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo madiwani kuhusu taratibu za usajili wa biashara, utoaji wa leseni pamoja na ulinzi wa haki miliki, ili waweze kuwasaidia wafanyabiashara katika kata zao kwa ufanisi zaidi.
Hata hivyo amempongeza Meya wa Jiji la Dodoma kwa kushiriki mafunzo hayo, hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya biashara katika mji mkuu wa nchi. Pia ametambua mchango wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma chini ya uongozi wa Rosemary Senyamule kwa ushirikiano wake katika kutoa elimu ya biashara na msaada wa kitaalamu.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanahusisha maeneo muhimu kama usajili wa kampuni, majina ya biashara, alama za biashara, hati miliki (patents), pamoja na utoaji wa leseni za viwanda na leseni za biashara daraja la “A”.
Aidha, amebainisha kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, BRELA imefanya maboresho mbalimbali ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara, ikiwemo kuanzisha mifumo ya kidijitali inayowezesha huduma kupatikana mtandaoni kupitia simu za mkononi.
Hata hivyo, Nyaisa ametaja changamoto ya utofauti katika utoaji wa leseni za biashara katika ngazi za serikali za mitaa. Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara hupewa leseni daraja la “B” badala ya “A” kimakosa, hali inayosababisha mkanganyiko.
Amewataka madiwani kutumia mafunzo hayo kutatua changamoto hizo na kuwa mabalozi wa kuhamasisha urasimishaji wa biashara, hususan kwa vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo.
“Baada ya mafunzo hayo, tunatarajia muwe mabalozi wazuri katika maeneo yenu na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika ngazi za chini,” amesema.
Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwona Chaula,amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea uwezo madiwani wanaofanya kazi kwa karibu na wananchi katika ngazi ya msingi. Aliongeza kuwa yatawasaidia kuelewa vyema taratibu za usajili na utoaji wa leseni za biashara ili waweze kuwasaidia wananchi katika shughuli zao za kila siku za kiuchumi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa BRELA wa kujenga uchumi shindani na jumuishi kwa kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli rasmi za biashara nchini.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe Alimwona Chaula,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya madiwani wa Halmashauri ya Dodoma yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) yakilenga kuwajengea elimu juu ya Huduma zitolewazo na BRELA katika kuwezesha biashara nchini yaliyofanyika leo Aprili 15,2026 jijini Dodoma

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) Bw Godfrey Nyaisa,akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa Halmashauri ya Dodoma wakati wa mafunzo kwa madiwani hao juu ya Huduma zitolewazo na BRELA katika kuwezesha biashara nchini. Mafunzo hayo yametolewa na BRELA yaliyofanyika leo 15,2026 jijini Dodoma.

Madiwani wa Halmashauri ya Dodoma wakisikiliza elimu juu ya Huduma zitolewazo na BRELA katika kuwezesha biashara nchini. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea ufahamu juu ya masuala ya urasimishaji biashara ili kuleta chachu za mabadiliko katika Kata wanazoziongoza. Mafunzo hayo yametolewa na Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) leo Aprili 15, 2026 jijini Dodoma

Madiwani wa Halmashauri ya Dodoma wakisikiliza elimu juu ya Huduma zitolewazo na BRELA katika kuwezesha biashara nchini. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea ufahamu juu ya masuala ya urasimishaji biashara ili kuleta chachu za mabadiliko katika Kata wanazoziongoza. Mafunzo hayo yametolewa na Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) leo Aprili 15, 2026 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kampuni na Majina ya Biashara Bw Isdor Nkindi, akitoa elimu kwa Madiwani wa Halmashauri ya Dodoma juu ya Huduma zitolewazo na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Mafunzo hayo yametolewa na BRELA yaliyofanyika leo Aprili 15, 2026 jijini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Paschal Inyasi Chinyele,akichangia mada wakati wa semina ya madiwani wa Halmashauri ya Dodoma yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) yakilenga kuwajengea elimu juu ya Huduma zitolewazo na BRELA katika kuwezesha biashara nchini yaliyofanyika leo Aprili 15,2026 jijini Dodoma.

Madiwani wa Halmashauri ya Dodoma wakichangia mada juu ya Huduma zitolewazo na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika kuwezesha biashara nchini katika semina iliyoandaliwa na BRELA leo tarehe 15 Aprili, 2026 jijini Dodoma