Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Chama Kikuu cha Wakulima Mara Cooperative Union (WAMACU), kimewakumbuka wakulilima wa zao la mahindi hii ni kufatia kuwepo na soko duni la zao hilo ambalo ni moja ya mazao ya biashara yanayozalishwa Mkoani Mara .

Akizungumza na waandishi wa jabari Meneja wa Bodi ya Kahawa ya WAMACU, Samweli Gisiboye amesema lengo ni kuwainua wakulima wa chini kwa kuwatafutia soko pamoja na pembejeo za kilimo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao bora.

Amesema katika kuhakikisha wakulima wanaendelea kuhitaji na kutumia pembejeo ni lazima wawatafutie soko la mtandani kwa mfano wakati nchi jirani ya Kenya inauza kilo 1000 kwetu iwe ni 1200.

Akiendelea kuzungumza amesema huu ni mpango mkakati wa chama hicho kuwa na dira halisi kulingana na maelekezo ya serikali kuwasajili wakulima na kuhakikisha wanapata masoko ya mahindi ili kuleta tija kwa kuwa na mbolea pamoja na mbegu.

Aidha huduma hii inatakiwa kumgusa kila mkulima wa chini kwa kuhakikisha anapata mbolea,mbegu na baada ya kuzalisha apate soko la uhakika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya kahawa Mzee David Hechei amesema kiwanda cha kahawa kinasaidia kujikwamua katika uchumi.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kumsogezea mkulima huduma karibu na kuwaomba Wakulima kukithamini kiwanda hicho maana ni mali yao.

Hata hivyo hakusita kuwapongeza waamdishi wa habari kwa namna wanavyoshirikiana kukitangaza kiwanda cha kahawa kwa shughuli kinazoendesha na kuongeza kuwa hata kukosolewa pale wanapokosea ni fursa .

WAMACU imefanikiwa katika msimu 2023/2024 kufanya ukoboaji wa kahawa ya maganda katika kiwanda kipya na zoezi la ukoboaji linaendelea hadi kufikia Desember 2023; kilo 246,953 zimekolewa na kupatikana kg 124,646 za kahawa safi sawa na asilimia 50.

Katika msimu wa 2023/2024 Wamekusanya jumla ya kilo 571,747 kutoka vyanzo vya Wilaya ya Tarime mjini pamoja na Tarime Vijijini ambapo kg 47,098 zimetoka JKT Ng’ereng’ere Tarime Vijijini na vilivyosalia ni kutoka maeneo mengine ya Tarime mjini na ya Mkoa wa Mara .

WAMACU walinunua kiwanda cha kahawa kwa gharama ya zaidi ya milioni 603. Aidha wametumia zaidi ya milioni 611 katika kugharamia ujenzi wa miundo mbinu.

Mpaka sasa WAMACU ina mafanikio na mtaji wa julma ya shilingi billion 4,223,535,44 katika Ardhi,majengo.maghala ya kuhifadhia nafaka pamoja na hisa za Wanachama.

Please follow and like us:
Pin Share