Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewataka wakulima kununua mbolea kulingana na mahitaji yao kwani hakutakuwa na upungufu wa bidhaa hiyo kwa msimu wote wa kilimo wa 2022/2023.

Ametoa kauli hiyo jana Septemba 2, 2022 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua shughuli ya upakuaji wa mbolea unaoendelea katika bandari ya Dar es Salaam.

Amesema meli ya MV Clipper Clyde inaendelea kupakua tani elfu thelasini na moja (31,000) za mbolea ya kupandia aina ya DAP za kampuni la mbolea la OCP.

Wakati huohuo waziri Bashe ameeleza kuwa kiasi cha tani laki moja na nusu (150,000) cha mbolea kipo katika maghala mbalimbali nchini mbolea nyingine ikitarajiwa kufikishwa nchini mwezi Oktoba na mwezi Novemba.

Waziri Bashe amewaeleza wakulima kuwa ruzuku ya mbolea si ya muda mfupi itadumu mwanzo mpaka mwisho wa msimu na hivyo hakuna haja kununua mifuko mingi ya mbolea na kuihifadhi majumbani.

“Hakutakuwa na upungufu wa mbolea ni heri hiyo pesa utumie kwa matumizi mengine hata yale ya kuongeza eneo la kilimo” alisisitiza Bashe.

Pamoja na hayo Waziri Bashe amewataka wakulima kutoa taarifa sahihi kwenye zoezi la usajili wa wakulima linaloendelea.

“Baadhi ya wakulima wameanza kutoa taarifa za uongo, niwaombe wakulima mtoe taarifa sahihi kwani huko mbele tutatumia GPS cordinate kutambua maeneo ya mashamba mliyoyaandikisha hivyo ni vema kuwa na taarifa sahihi” alikazia Bashe.

Aidha, waziri Bashe amezishukuru kampuni zote zinazoingiza mbolea nchini na kueleza Serikali itahakikisha zinapata malipo ya ruzuku kwa wakati.

Amesema, Rais Samia ametuagiza kuhakikisha tunajenga mfumo mzuri wa biashara ili kuwezesha serikali kufanya biashara na sekta binafsi.

Amewataka wakala wote wa mbolea kuhakikisha wanafuata utaratibu wa uuzaji wa mbolea za ruzuku kwa kuhakikisha mifuko inayotumika kuwekea mbolea ina QR code na imechapishwa neno ruzuku ili kuondoa mambo ya kubandika stika.

Mwisho waziri Bashe amesema “Tutaendelea kujenga mifumo ya kilimo ni biashara. Tunataka wakulima wazalishe kwa tija tunataka kutengeneza

By Jamhuri