Na Zulfa Mfinanga, JamhuriMedia, Arusha
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewapongeza wajumbe wa ALAT kwa kuwa kinara katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa nchini.
Dkt. Nchemba amezungumza hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa ALAT unaofanyika jijini Arusha uliowakutanisha Wenyeviti, Mameya pamoja na Wakurugenzi.
“Mchango wenu unaonekana kwa usimamizi wenu katika kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa na miundombinu ya kutosha, shule za amali 103 kwa mpigo, katika mikoa mbalimbali, vyuo vya ufundi na shule za msingi na skondari pamoja na vituo vya afya”
Amesema ndani ya mwaka mmoja wataenda kutekeleza jukumu la elimu ya lazima kwa miaka kumi ambapo kwa mwaka 2028 wanafunzi milioni 13 wataingia kidato cha kwanza zoezi litakalogharimu bajeti zaidi ya Trilion 1,
“Rai yangu kwenu mi kuongeza jitihada za kuongeza mapato, kuongeza bima ya afya kwa wote, katika kipindi ambacho tunaenda kuanza Dira mpya, kudhibiti ufujaji wa mapato ili kuwa na uelekeo ulio sahihi.





