Timu ya Yanga SC imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi kuinoa timu hiyo msimu ujao akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba wake.

Kocha huyo raia wa Argentina ametambulishwa leo Juni 24 na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati wa mkutano mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

Gomondi mwenye uzoefu na soka la Afrika kwa zaidi ya miaka 20 amewahi kuzifundisha timu mbalimbali ikiwemo Mamelodi Sundown (Afrika Kusini),USM Alger ya Algeria na Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco.

By Jamhuri