Ziara ya katibu Mkuu CCM Chongolo wilayani Lushoto

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo akionyesha jambo kwenye mchoro wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli wakati wa ziara yake katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, ikiwa muendelezo wa ziara zake za kukagua uhai wa Chama na Kukagua,Kusimamia na Kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo akipata maelezo ya mchoro wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli kutoka kwa Msanifu wa Majengo Yassin Mringo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo akihutubia  wanachama na wakazi wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani Tanga ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama na Kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya  mwaka 2020-2025.