Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA Dar es Salaam

Ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika nchi za Morocco na Saudia Arabia zimeleta manufaa na tija kubwa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo  mifugo, nishati, ajira  na uwekezaji.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya hiyo wameyaeleza hayo  leo  katika  Mkutano huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo, Novemba 15, 2023.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus akielezea ziara hiyo katika nchi za Morocco na Saudi Arabia aliyoifanya Novemba 08 hadi 11, mwaka huu amesema Rais Samia alishirki kwenye Jukwaa la Wawekezaji barani Afrika uliofanyika Jijini Marackesh Morocco.

Lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni kutafuta fedha za ufadhili miradi na miundombinu yenye sifa za uwekezaji ili kuhamasisha sekta binafsi ziwe zinachangia na kuwakutanisha wadau mbalimbali.

Amesema kuwa Rais Samia alishiriki pia Mkutano wa Saudi Arabia na nchi za Afrika uliofanyika Riyadh ambapo  taasisi ya kimaendeleo ya Saudi Arabia Iimewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 533 kwenye matiafa ya Afrika ikiwemo Tanzania.

 “Kampuni ya Almaray iko tayari kuja nchini kwa ajili ya kuanziasha uzalishaji wa majani ya kulisha mifugo, Kampuni hiyo tayari imeshaanziasha mazungumzo na wizara hiyo. Kampuni nyingine ambayo imeonyesha nia ni Salic ambayo inaitwa Crown Agricultural ambayo nayo inalenga kuanzisha uzalishaji wa majani ya kulisha mifugo mradi wa  kunenepesha ng’ombe  na pia kuuzwa katika soko la Mashariki ya Kati.” Amesema Zuhura Yunus

Aidha Zuhura Yunus amesema, katika ziara hiyo  nchi hizo mbili zimetia saini hati za  makubaliano kwenye eneo la wafanyakazi wa ndani vile vile kwenye eneo la nishati na Tanzania imefanikiwa kupata mkopo wa Dola Milioni 32  kwa ajili ya umeme huko Benako Kyaka.

Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega amesema ziara anazozifanya Rais Samia zinaleta tija, kwa maana Dunia ya sasa hakuna tena  haja  kujifungia hivyo inahitaji ushirikiano ili  utangaze fursa zinazopatikana  katika taifa lako.

“Tanzania kuna vivutio vya utalii, madini na rasilimali nyinginezo lazima wavitangaze ili waweze kuja kununua na kutalii, hivyo wanatarajia Shirika la Ndege nchini (ATCL) na la Saud Arabia kujenga ushirikiano wa karibu.”Amesema

Akizungumzia kuhusu kuongeza uzalishaji wa nyama, Ulega amesema Tanzania imeongeza usafirishaji wa nyama kutoka tani 1700 hadi kufikia tani 14000  katika mauzo ya nje ya nchi ambapo Saudi Arabia kwa mwaka huu wamenunua tani 1400 kwa mwaka huu na ni fursa kubwa hivyo wapo tayari kushirikiana na Tanzania.

“Asilimia 80 ya nyama iliyouzwa nje ya nchi ni mbuzi na kondoo, kwa upande wa nyama ya ng’ombe bado haijakidhi ubora na kuna changamoto, tunahitaji mjadala kwa sababu mifugo ni utajiri lazima iende sokoni kwa sababu inachangia asilimia saba ya pato la taifa”Amesema

Amesema kuna tatizo la magonjwa ya mifugo hivyo wanatarajia kufanya kampeni ya uchanjaji wa mifugo kila mfugaji kuchanja kwa ratiba maalumu itakayowekwa kama ilivyo kwa binaadamu ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Samia.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Fedha  na Mipango Zanzibar  Dkt. Saada Mkuya amesema ziara zinatoa fursa ya kukutana na wawekezaji na mashirika mbalimbali ambayo wanashirikiana nayo katika kutekeleza miradi ya fedha nchini.

Akielezea mradi wa bandari ya Mwangapwani ambayo ni bandari kubwa na jumuishi ambayo itakuwa ni bandari ya Makontena, Oili na gesi lakini pia na sehemu ya abiria pia kutakuwa na eneo chelezo la watoa huduma za meli.

“Tulivyokuwa Morocco wame deal na kontena, tunavyojua nchi kama Zanzibar uchumi wake unategemea mafanikio ya bandari kwa hiyo kwetu sisi katika miradi ambayo  ni kipaombele  ni bandari pamoja na miundombinu barabara ambayo  itaunganisha zile bandari kwa hiyo tuanza nabandari ya makontena bandari ya mizigo bandari itakuwa tunaweza kuita bandari samart port,” 

 Amessama kupitia mradi huo watatengeneza ajira200 za moja kwa moja  kwa sababu itakuwa  inahusisha matumizi ya makubwa ya mashine lakini pia  inatarajia kutoa ajira zipatazo 1000.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshawekeza karibu Dola Milion 35 kwa ajili ya kuweka muindombinu ya msingi, serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ambazo ziatakuwa zianaingia ndani ya bandari yetu” Amesema Waziri Mkuya.

Aidha Waziri Mkuya amesema tayari wameanza upembuzi yakinifu kwaajili ya ujenzi wa ungwe ya kwanza ya bandari na tayari ambayo tayari Dola Milion 450 zimetolewa.

Akizungumzia suala la wafanyakazi za ndani nchini Saudi Arabia kutoka Tanzania Balozi wa Tanzania nchini humo John Kilima amesema eneo la mashariki ya kati kwa kiasi kikubwa ni tegemezi ya nguvu kazi kutoka nje ya eneo lake ambapo ameleza kuwa takwimu za idadi  ya watu wa nchi hizo kwa mfano Oman ina idadi ya watu wapatao Million tano, Milioni 2.4 ya idadi hiyo wakiwa wageni kutoka nchi za nje.

“Ukienda UAE inakwenda mpaka kufikia asilimia 50 ya idadi ya watu ni wageni wa ya nchi sasa hili limaonyesha kabisa kuwa wenzetu ni wategemezi wa nguvu kazi kutoka nje ya eneo lao, nguvu kazi za aina zote kuanzia skilled mpaka unskilled”Amesema Balozi Kilima.

Amesema Saudi Arabia sasa inajenga mji mkubwa wa kisasa wa kibiashara uitwao Niaum ambao umefikia asilimia 90 kukamilika ambapo mji huo una vitu vingi ikiwemo maduka na miradi mbalinbali ambayo itahitaji wafanyakazi ambapo kwa miaka ya nyuma mahitaji hayo yamekuwa yakikidhiwa nan chi za Asia na zile za mashariki ya mbali kama vile Indonesia Pakstani na India.

“Kumekuwa na swala ambalo limejengeka kupitia mitandao ya kijamii lakini pia ikiwemo vyombo vya habari kwamba watu wengi wanateseka wakiwa uarabuni, naweza kusema ni asilimi 92 habari hizi si za kweli, ni kwamba wapo watu wanafanya kazi katika mazingira mzuri na kipato wanachopata ni kikubwa”

Balozi  Kilima amesema kwa pande wa Oman watanzania wapatao 25000 wanafanya kazi ambapo kati yao Zaidi ya 17000 wanafanya kazi za ndani hivyo uwepo wao kwa wingi ni ushahidi tosha kwamba wanafanya kazi katika mazingira mazuri.

“Lazima nikiri na ndiyo maana nikasema kwamba asilimia 92 habari hizo siyo za kweli nimeweka asilimia 08, katika hiyo asilimia 08 tunakubali kwamba ziko changamoto ambazo ni a kawaida  na changamoto hizi nyingi zinazowakuta  ni kwa wale wengi ambao wamepita bje ya mfumo ambao uiliwekwa.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema ujenzi  wa reli  kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro umekamilika  kwa kiasi kikubwa ukiacha na sehemu chache ambazo bado hazijakamilika kwa mfano katika eneo la vingunguti nyerere pamoja na Banana.

“Kitu ambacho kilikuwa kimetusimamisha kwa mda ni vichwa, tulikuwa hatujapata vichwa sasa hilo linaweza likawa na maelezo mengi sana kwa nini vichwa vimechelewa, lakini tmekuwa na changamoto hiyo ya kutoukpata vichwa vya treni “Amesema Kadogosa

Aidha Masanja amesema kwa sasa TRC wako katika hatua ya kuvifanyia majaribia vichwa hivyo katika hatua mbili ili kupima ufanisi na mwendo wa kusafiri kwa mwendo wa kilimita moja kwa saa.

Akizungumzia sula la uwekezaji Mkurugenzi wa uhamasishaji na Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mathew Mnali amesema suala la uwekezaji kila nchi lina taratibu za uwekezaji mitaji mingi kutoka katika nchi zilizoendelea.

“Suala la kutafuta uwekezaji ni suala laushindani ni eneo muhimu TIC tunapata njia rahisi kuleta wawekezaji ambapo Januari hadi Septemba miradi 137 ilisajiriwa ukilinganisha na miradi 89 iliyokuwepo mwaka jana takribani ajira 12000  ziliongezeka “ Amesema Mnali