Monthly Archives: April 2019

Miaka 35 bila Sokoine

Alasiri ya Aprili 12, 1984 wakati huo nikiishi Kurasini Highway, nilivuka barabara kwenda Kurasini Shimo la Udongo kuchukua picha zangu za passport kwenye studio moja. Jina la hiyo studio silikumbuki, maana miaka 35 ni mingi, lakini nakumbuka ilikuwa karibu na duka maarufu la ndugu mmoja aliyeitwa King Nose, jirani na Mti Mpana. Nilipovuka barabara na kuyakaribia maduka ya eneo hilo, ...

Read More »

Ubakaji na utelekezaji wa watoto

Kuna jambo ambalo limezungumziwa bungeni na kunifanya nihisi furaha iliyopitiliza. Jambo hilo ni kwamba wanandugu ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kosa la watu kuwabaka hata dada zao na wakati mwingine binti zao, pia kuwatelekeza watoto wanaotokana na unyama huo wa hatari! Itakuwa ni jamii ya aina gani tuliyomo tunapoyaacha majanga ya aina hiyo yaendelee kutamalaki ndani yake! Tulizoea kusema haya ...

Read More »

Mwanadamu na fikra zake 

Mwanadamu ana uwezo wa kufikiri na kuamua kutenda jambo zuri au baya. Anaweza kujifanyia haya binafsi, kuwafanyia wanadamu wenzake na viumbe vyote vilivyomo katika ulimwengu huu, kwa nia tu ya kuridhisha nafsi yake. Na hapa ndipo yanapoanzia maelewano na mifarakano baina ya wanadamu. Uwezo alionao mwanadamu huyu unampa kiburi kutii au kutotii jambo, kukiuka kanuni na taratibu alizojiwekea na zile ...

Read More »

Yah: Dunia inakwenda kasi, naomba nishuke

Naanza na salamu kama ilivyo kawaida yangu, naamini huo ni moja ya uzalendo ambao tumekuwa nao kama watoto wa Tanganyika mpaka ikawa Tanzania huru. Salamu inakufanya umtambue mzalendo mwenzako na kumtambua kama yuko salama na uko mikono salama kama mmekutana barabarani. Nakumbuka enzi hizo tukihisi tu kama si mwenzetu kwa hatua ya salamu tu, tunaanza kwa kukuomba barua ya mwenyekiti ...

Read More »

Buriani Lutumba Simaro Massiya

Lutumba Simaro Massiya aliyekuwa mtunzi na mcharazaji maalumu wa gitaa la ‘rhythm’ katika bendi za T.P. OK Jazz na Bana OK, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amefariki dunia Machi 30, mwaka huu katika Jiji la Paris, Ufaransa. Taarifa hiyo ilitangazwa na mwanawe wa kiume, Simon Lutumba, kutoka jijini Paris, kwamba baba yake Lutumba alifariki dunia akiwa na umri wa ...

Read More »

Simba SC ni ‘half time’

Dakika 90 kati ya 180 za mchezo wa robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika baina ya Simba SC na TP Mazembe zimekamilika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa miamba hao kutoka suluhu. Klabu ya Simba imekuwa ikiheshimika huko nje kwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani, hasa ikikumbukwa kwamba ilipata matokeo chanya dhidi ya ...

Read More »

Mkakati kuing’oa CCM mwaka 2020

Mnyukano wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza. Vyama 10 vya upinzani vimeandaa mkakati wa kisayansi kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutumia Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2018. Kwa upande wake, CCM imejigamba kuwa maisha ya vyama vya upinzani katika uwanja wa siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao nchini ni ‘mahututi’. Gazeti la JAMHURI linafahamu kwamba vyama ...

Read More »

Ecobank yamwibia mteja mamilioni

Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia huduma ya internet banking na kuziingiza katika akaunti iliyoko nchini Afrika Kusini. Hukumu hiyo ya kesi namba 68 ya mwaka 2014, imetolewa na Jaji Barke Sehel. Inahusu ...

Read More »

Rais ampandisha cheo aliyekataa rushwa

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, ameteuliwa kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imesema uteuzi huo uliofanywa na Rais John Magufuli, umeanza Machi 31, mwaka huu. Desemba, mwaka jana, Gazeti la JAMHURI liliandika habari iliyohusu Mbibo kukataa rushwa. Baadaye Januari, mwaka huu ...

Read More »

KNCU, Lyamungo AMCOS wavutana umiliki shamba la kahawa

Mvutano mkali umeibuka baina ya Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Lyamungo kuhusu umiliki wa shamba la kahawa la Lyamungo kutokana na kila upande kudai ni mmiliki halali. Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 112 lililopo Lyamungo, Wilaya ya Hai limekuwa katika mgogoro usiokwisha kwa muda wa miaka 16 hadi sasa, hivyo ...

Read More »

Serikali yashitukia ufisadi wa milioni 71/-

Serikali imeshitukia matumizi mabaya ya fedha za makusanyo ya ardhi kiasi cha Sh milioni 71. Fedha hizo zinazodaiwa kutojulikana zilipo zinatokana na malipo ya viwanja 194 vya wakazi wa mji wa Hungumalwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza. Raia hao walitoa fedha hizo ili wapimiwe na kupewa hati za maeneo yao ya makazi na biashara. Naibu Waziri wa ...

Read More »

Msajili wa Vyama awe mlezi wa vyama

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa tishio la kukifuta Chama cha ACT-Wazalendo. Sababu kadhaa zimetolewa, zikiwamo za madai kwamba chama hicho kinatumia udini na kinaharibu kadi na mali za chama kingine – CUF. Tunaandika haya kwa unyenyekevu mkubwa tukitambua kuwa dola na vyombo vyake vina dhima ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na salama. Kwa kulitambua hilo, ...

Read More »

NINA NDOTO (13)

Anza na ulichonacho, anzia hapo ulipo   Anza na ulichonacho. Anzia hapo ulipo. Kusubiri kila kitu kikae sawa ndipo uanze ni kuchelewesha ndoto zako. Kusubiri kila kitu kikamilike ni sawa na kusubiri meli kwenye kiwanja cha ndege. Muda sahihi wa kuanza kuishi ndoto zako ni leo, wala si kesho, kesho kutwa au wiki ijayo. Mwanamuziki Ben Pol aliwahi kuimba akisema: ...

Read More »

Tuoteshe miti ya asili

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema. Ni jambo la kushukuru sana. Wakati tulipopata uhuru mwaka 1961 nchi yetu iliitwa Tanganyika, lakini baada ya kuungana na Zanzibar Aprili 26, 1964 ikajulikana kama Tanzania. Kabla ya utawala wa Waingereza eneo la Afrika Mashariki, zikiwamo Burundi, Rwanda, Tanzania Bara na Buganda; kuanzia mwaka 1885 hadi mwaka 1919 yalikuwa chini ya utawala wa ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (8)

Wiki iliyopita niliahidi kujibu maswali haya: “Je, unafahamu utaratibu wa kisheria wa kusajili Jina la Biashara, gharama ya usajili, muda wa kukamilisha usajili, nyaraka zinazotakiwa, umri wa mtu anayetaka kusajili Jina la Biashara na matakwa mengine ya kisheria? Usikose nakala yako ya Gazeti hili makini la uchunguzi la JAMHURI Jumanne ijayo.” Sitanii, baada ya makala hii, nimepata maombi mengi. Nimepata ...

Read More »

Ujira wa wafunga maturubai malori ya makaa ya mawe matatani

Vibarua wa kufunga maturubai mizigo ya makaa ya mawe kwenye malori wamevurugana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kujitwalia mamlaka ya kutunza fedha zao katika akaunti ya halmashauri. Kwa mujibu wa vibarua hao kutoka Kata ya Amanimakolo, wilayani Mbinga, ili kulipwa stahili zao ni lazima kwanza kipatikane kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na zaidi ...

Read More »

TIC, halmashauri kuvutia wawekezaji

Utekelezaji wa sera ya taifa inayoelekeza halmashauri zote nchini kutenga rasmi maeneo maalumu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika kila halmashauri nchini bado unasuasua na kusababisha kero kwa wawekezaji wa nje na ndani. Sera hii ilikusudia kurahisisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wawekezaji, kwa mkakati wa kupunguza usumbufu na  kuchelewa kupata hatimiliki kwa kutumia utaratibu wa kawaida. Serikali ...

Read More »

Maswali ni mengi hukumu ya kifo kwa Mwalimu Respicius

Siku niliposikia Mahakama Kuu (Bukoba) imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa Mwalimu Respicius Patrick kwa kosa la kumuua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius, niliduwaa. Katika kuduwaa, nilianza kutafakari juu ya ndoto yangu hii ya kuwa mwalimu niliyoipigania kwa nguvu zote, kwa uwezo wa Mungu, na hatimaye kufanikiwa. Ni kwamba nikiwa mwanafunzi ndoto ya kuwa mwalimu au ...

Read More »

Ndugu Rais, kati ya nguo na pasi kipi kinapigwa pasi?

Ndugu Rais, tunasoma katika kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu kuwa: “Wananchi wanataka rais awathamini raia waandamizi waliokamilisha wajibu wao na kustaafu katika ujenzi wa taifa ili wasipate shida katika wakati wao wa kutokuwa na nguvu za kuendelea kujikimu. Hivi sasa wastaafu wanaishi katika uchochole wa kutisha. Pensheni yao ni ya kijungujiko.” Tukiwa katika uelewa huu, naona ni vema nikufikishie ...

Read More »

Wanasiasa si wenzetu

Wanasiasa siyo wenzetu kwa maana nyingi tu, na siyo kwa sababu tu ya kuitwa waheshimiwa. Kwanza, ni watu wenye kujiamini, wenye imani inayoambatana na uwezo mkubwa wa kusikia maoni tofauti kabisa na ya kwao, lakini wakaendelea kushikilia msimamo kuwa wanachofanya ni sahihi, na kuamini kuwa malengo yao ndiyo muhimu zaidi. Utampambanua mwanasiasa kwa ubishi. Ubishi si jambo baya kama kusudio ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno

Majivuno yaliwabadili malaika wakawa mashetani. Unyenyekevu huwafanya watu wawe kama malaika – Mt. Augustino. Kitendawili: Tega! ‘Ananifanya nichukiwe na kila mtu’. Jibu ni ‘majivuno’. Kitendawili: Tega! ‘Nikimmeza najisikia sana’. Jibu ni ‘majivuno’. Majivuno ni jeraha lisiloponyeka katika maisha. Majivuno ni jeraha linalonuka kama mzoga wa porini. Ni donda ndugu. Majivuno ni dereva wa shetani. Mwaka 2013, Jarida la ‘New People’ ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (23)

Kataa kujikataa Kukataa kujikataa ni mtihani. Kujikataa ni kujihisi wewe si mtu muhimu. Ukweli wewe ni mtu muhimu. “Kukosa kitu cha kukufanya ujisikie wewe ni mtu muhimu ni jambo liletalo huzuni mkubwa sana, ambalo mtu anaweza kuwa nalo,” alisema Arthur E. Morgan. Kumbuka wewe si bahati mbaya. Wewe ni wewe. Hakuna ‘spea’ kwa ajili yako. Uliletwa duniani kwa lengo maalumu. ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons