Daily Archives: May 21, 2019

Masele yametimia

Hatima ya Stephen Masele kuendelea au kutoendelea kuwa mbunge katika Bunge la Afrika (PAP) inajulikana wiki hii. Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekaliwa vibaya kisiasa, na aliyeshika mpini kwenye vita hiyo ni Spika Job Ndugai ambaye naye anatoka katika chama hicho. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa ni Makamu wa ...

Read More »

Mochwari ya Muhimbili mmmh!

Mpita Njia (MN) kwa umri alionao, anaona kuna haja ya kuyakaribia Maandiko Matakatifu na kuyaishi. Kwa umri wake amepitia mengi, lakini la hivi karibuni la kuingia katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili limemfanya azidi kuimarika kiimani. Ni kwa sababu hiyo MN ameanza kukariri baadhi ya vifungu. Baada ya kufika Muhimbili, akarejea maandiko katika Kitabu cha Ayubu ...

Read More »

Mazito aliyekwepeshwa kwa Magufuli

James Kunena aliyeporwa nafasi ya kuzawadiwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa mfanyakazi bora wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) alipigiwa kura na wenzake kwa kuwa alibuni vipuri vilivyotakiwa kuagizwa nje ya nchi. Hatua yake hiyo iliwashawishi wenzake kumchagua kuwa mfanyakazi bora lakini nafasi hiyo akapachikwa Focus Sahani ambaye hakustahili nafasi hiyo. Kutokana na hali hiyo, fukuto limezidi kuibuka miongoni ...

Read More »

Abambikiziwa uanachama mfuko wa jamii

Uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa miaka minne umeshindwa kulipa mafao ya kustaafu ya askari polisi aliyelitumikia jeshi hilo kwa miaka 33, kisa kabambikizwa uanachama katika mfuko mwingine. Thomas Njama, amestaafu Jeshi la Polisi mwaka 2015 akiwa Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu mkoani Arusha. Amesema PSPF wanatakiwa kumlipa kiinua mgongo cha Sh 47,162,022 na ...

Read More »

Mwalimu mtuhumiwa mauaji ni Mkenya

Shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Himo, Moshi mkoani Kilimanjaro inatuhumiwa kuajiri mwalimu raia wa Kenya asiyekuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Mwalimu Laban Nabiswa, ni mshtakiwa wa tatu katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule hiyo ya Scolastica. Laban amekiri mahakamani kuishi na kufanya kazi nchini isivyo halali ...

Read More »

Rushwa ya ngono yamtumbukia mwalimu

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jabarhila, iliyopo Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Mwatanda Omari (37), amehukumiwa kwenda jela miezi 12 kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono. Mwalimu Omari alitenda kosa hilo Machi 9, 2017 kwa kumuomba rushwa hiyo mzazi wa mwanafunzi katika shule hiyo. Jina la mzazi limehifadhiwa. Mzazi alikuwa anaomba uhamisho wa mtoto kutoka shuleni hapo kwenda Dar es ...

Read More »

Busara itumike TRAWU

Wiki iliyopita Gazeti hili la JAMHURI lilichapisha habari kuhusu kashfa iliyojitokeza wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi, kwa mwaka huu yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kashfa hiyo imekikumba Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Ndani ya chama hicho, baadhi ya viongozi wake wanadaiwa kuwasilisha jina la kigogo asiyestahili kuwa mfanyakazi bora ili apewe mkono na ...

Read More »

NINA NDOTO (18)

Taa nyekundu na kijani za maisha   Zamani nilipokuwa nikisafiri na kupita katikati ya jiji palipokuwa na taa na kukuta taa nyekundu inawaka nilikasirika. Nilitamani muda wote taa ya kijani iwake ili tupite. Siku hizi nikifika na kuona taa nyekundu inawaka nafurahi na kuona inaelezea hali halisi ya maisha. Tupo katika zama ambazo kila mtu anataka kila kitu anachokifanya kifanikiwe ...

Read More »

Tumlilie mzee Mengi tukitafakari maneno yake

Hakuna mtu anayeweza kuandika yote ya Dk. Reginald Mengi. Hata watu alioshinda nao na kukaa nao kwa miaka mingi, hawawezi kuyaeleza yote.  Huyu alikuwa mtu wa kitaifa na kimataifa. Alikuwa mtu wa watu wote, wadogo, wakubwa, maskini, walemavu, matajiri, wanasiasa hata na watu wa vijiweni. Alizalisha ajira kwa Watanzania na watu wengine kutoka nje ya nchi. Alikuwa mcha Mungu, mshauri ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (14)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuhoji iwapo unazifahamu nyaraka tatu muhimu unazopaswa kuwa nazo baada ya kusajili kampuni. Nyaraka hizi nimepata kuzigusia katika makala zilizotangulia na hata nilipozungumzia Jina la Biashara nilizigusia. Kabla sijaingia kwa kina kuzungumzia nyaraka hizi, naomba kuwashukuru wasomaji wangu wengi mnaonipigia simu kutoka Muheza, Bukoba, Mbeya, Kigoma, Mwanza, Zanzibar, Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, ...

Read More »

‘Bila elimu – dini tutakwama’

Miaka 20 kifo cha Mwalimu Nyerere Mei 16, mwaka huu Chama cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) ambacho ni chama cha kitume ndani ya Kanisa Katoliki kiliandaa kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Dhamira ya kongamano ilikuwa Maendeleo Jumuishi na yenye kujali ustawi wa maisha ya wananchi. Mada mbalimbali zilijadiliwa. Washiriki walitoka makundi na ...

Read More »

Bandari inafanya kazi saa 24

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikiana na wadau wake wa bandari imeboresha na kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wake katika Bandari ya Dar es Salaam. Uboreshaji huo umefanyika na unaendelea kufanyika kwa sababu bandari ni lango kuu la biashara kwa nchi yetu na nchi zote zinazotumia bandari hii kubwa hapa nchini. Kati ya mambo yaliyoboreshwa na yaliyorahisishwa ...

Read More »

‘Wosia’ wa Dk. Reginald Mengi

Jumanne, Mei 7, mwaka huu maelfu ya Wana Dar es Salaam walikusanyika katika Ukumbi wa Karimjee kuaga mwili wa mpendwa wetu Dk. Reginald Mengi. Runinga za ITV, Star TV, Channel 10, Clouds TV, televisheni za mitandao ya kijamii na redio mbalimbali zilionyesha na kutangaza shughuli ile mubashara. Mmoja ya wazungumzaji siku ile alikuwa James Mbatia. Wakati anazungumza alisikika akitamka kuwa ...

Read More »

Ndugu Rais hakuna aliyeumbwa kwa bahati mbaya

Ndugu Rais, mwanetu Atosha Kissava katika wimbo wake wa Moyo wangu, aliimba, “Moyo wangu utakusifu wewe Baba, utakusifu milele! Najua uliniumba nitimize kusudi lako Baba. Siko hapa kwa bahati mbaya’’, yuko Mtanzania mwenzetu ambaye kwa asiyemjua, kwa jina lake peke yake hawezi kujua kama ana dini au la, amesema Serikali imewasilisha katika Mahakama ya Rufani kusudio la kukata rufaa kupinga ...

Read More »

Mrejesho makala ya “Mwalimu angekuwepo angesemaje?”

Jumanne, Mei 7, 2019, wakati nimeketi kibarazani kwangu nasoma Gazeti la JAMHURI, Toleo Namba 397 la tarehe 7 – 13 Mei 2019, alikuja jirani yangu anaitwa Imma, kijana wa miaka 25. Kabla sijamwonyesha nilichokuwa nasoma, nikamuuliza: “Unadhani Mwalimu Nyerere angekuwepo akaona utendaji wa Rais Magufuli angesemaje?” Haraka, haraka akajibu: “Angempongeza sana!” Siku hiyo na siku zilizofuata niliendelea kupigiwa simu na ...

Read More »

Wanaotaka kufika kileleni Kilimanjaro wasibebwe

Nimesikia Serikali inatathimini kuweka cable car kwenye Mlima Kilimanjaro ili kuwafikisha wageni kileleni kwa haraka. Cable car ni mfumo wa usafiri unaobeba abiria kwenye behewa dogo linalosafiri kwa kuning’inia kwenye waya zilizopitishwa kwenye nguzo. Naamini zipo sababu nyingi nzuri za kuishawishi Serikali kuachana na wazo hili. Nitataja chache. Kwanza, kulinda ajira. Inakadiriwa watu 20,000 wanahudumia wageni wanaokwea Mlima Kilimanjaro na ...

Read More »

Kesi ya Sumry High Class, Manji

Moja ya faida kubwa ambayo huwavutia wengi kuacha kufanya biashara kama mtu binafsi na kuamua kufanya biashara kwa kutumia kampuni ni hii ya kuwa kampuni na mmiliki ni vitu viwili tofauti, hivyo kosa la kampuni halimhusu mmiliki na kosa la mmiliki haliihusu kampuni. Maana yake hata ukikopa kwa kutumia kampuni na ukashindwa kulipa, mali zako binafsi haziguswi isipokuwa za kampuni ...

Read More »

Kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa (2)

Mwandishi T. L. Osbon anasema: “Ukiacha kujifunza unaanza kufa.” Tafuta wazo jipya kila siku. Kumbuka usipotumia nguvu nyingi kuwaza mawazo yatakayoibadili dunia ni lazima utaajiriwa na watu waliotumia nguvu nyingi kuwaza mawazo yaliyoibadili dunia. Mwandishi wa vitabu vya kiroho, Tony  Evans anasema: “Watu wengi wanatumia muda wao mwingi kuishi maisha ya watu wengine.’’ Simamia ndoto yako. Huko Marekani msichana wa ...

Read More »

Kujua ni kinga ya majuto

Kujua ni mtihani. Majuto ni mjukuu kwa sababu kuna kutokujua. “Ningejua” huja baadaye. Ukijua huu, ule huujui, ukijua hiki, kile hukijui. Haitoshi kujua, lazima kujali. “Hakuna anayejali kiasi unachokijua, mpaka ajue kiasi unachojali,” alisema Theodore Roosevelt. Kujua ni mtihani. “Kujua unachokijua na ambacho hukijui, hiyo ndiyo elimu ya kweli,” alisema Conficius. Kuna ambao wako katika ndoa wanasema: “Ndoa yangu ningejua.” ...

Read More »

Tumekubali kuwa watu wa porojo

Hakuna wiki inayopita bila taifa letu kuingizwa kwenye mijadala. Mijadala yenye tija ni kitu cha maana. Shida ni pale tunapojikuta tukihangaishwa na mambo yasiyokuwa na faida yoyote – si kwa mtu binafsi wala kwa taifa letu. Kwenye mitandao ya kijamii tumesoma habari kuwa Serikali ya Kenya imesaini makubaliano na Serikali ya Afrika Kusini kwa ajili ya kupeleka walimu wa somo ...

Read More »

Masharti ya maendeleo

“Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi anaelewa masharti ya maendeleo, sharti moja kubwa ni juhudi. Sharti la pili la maendeleo ni maarifa. Juhudi bila maarifa haiwezi kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa.” Nimenukuu maneno haya kutoka katika Azimio la Arusha lililotokana na mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU, iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia ...

Read More »

Yah: Mambo ni mengi muda mfupi, Rais tusaidie

Lazima nianze na salamu na kongole kwa wote ambao mmefunga mwezi  huu mtukufu, ni kama vile tumepishana kidogo na wenzetu Wakristo ambao wametoka kufunga, hii ni neema na ninaamini kuna kitu chema kinakuja mbele kutokana na imani za kidini na waumini kuongezeka katika siku za hivi karibuni. Niwe mkweli kabisa kwamba imani ni kitu kizuri lakini inategemea imani yako umeiweka ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons