page za ndani

Aeleza alivyoua watoto Njombe

Kabrasha linaanza kufunguka juu ya nani anahusika na mauaji ya watoto mkoani Njombe huku ikithibitika kuwa ndumba, uchawi, ukimwi na ujinga vimekuwa nguzo ya mauaji hayo, JAMHURI limebaini. Ni wiki mbili sasa tangu matukio ya mauaji ya watoto wasiopungua saba katika mazingira ya kutatanisha na kutikisa taifa yaanze kutokea mkoani Njombe na JAMHURI limebaini namna baadhi ya matukio hayo yalivyotekelezwa. ...

Read More »

Polisi aiba bandarini

*CCTV Camera alizofunga Injinia Kakoko zamuumbua *Tukio lake lazua tafrani kubwa, IGP Sirro alishuhudia *Bandari sasa kama Ulaya, imefungwa kamera 486 *Polisi wafanya mbinu kumtetea mwenzao, wagonga mwamba Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam Mfumo mpya wa ulinzi aliouanzisha katika Bandari ya Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Deusdedith Kakoko, umemnasa askari Polisi aliyekabidhiwa jukumu la kulinda mali za bandari ...

Read More »

Botswana yanufaika madini, Tanzania yajikongoja…

*Waziri wao ashangaa Watanzania kutochukua fursa waliyoiomba *Ampongeza Rais Magufuli kubadili sheria za madini mwaka 2017 *Katibu Mkuu Madini asema Tanzania haina cha kujifunza Botswana Na Mkinga Mkinga, Aliyekuwa Gaborone, Botswana Wakati Tanzania ikibadili sheria yake ya madini mwaka 2017, Botswana mambo ni tofauti, nchi hiyo inaongoza kwa kuwa na sheria nzuri ya madini pamoja na namna wanavyonufaika na vipengele ...

Read More »

Matapeli wa bima waendelea kutamba

DAR ES SALAAM NA MWANDISHI WETU Kampuni zinazouza bima kwa magari yanayosafirishwa nje ya nchi (IT) zinaendelea kufanya biashara hiyo licha ya kubainika kuwa ni utapeli. Wakati Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ikisema stika za bima za muda kwa magari hayo zinapaswa kuuzwa Sh 28,000 kwa kila gari (ikijumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani –VAT), stika hizo zinauzwa ...

Read More »

Jaji Sumari majaribuni tena Moshi

Na Charles Ndagulla, Moshi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari, ameandamwa tena na wananchi wanaokataa asisikilize mashauri yaliyo mbele yake kwa madai kuwa hawana imani naye. Hatua hii inakuja huku kukiwa na taarifa kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Moshi kuwa jaji huyo yuko katika maandalizi ya kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. Ally Hussein ...

Read More »

Wakazi Dar kupata maji zaidi

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (Dawasa), Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, amewatoa hofu wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Pwani kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji. Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea miradi ya majisafi kwa ajili ya kujionea maendeleo ya ...

Read More »

Wizara isiwapuuze Botswana

Katika gazeti la leo tumechapisha habari za uchimbaji wa madini nchini Botswana na jinsi wakazi wa nchi hiyo wanavyonufaika. Tumempeleka mwandishi Botswana kufuatilia habari hizo na amekuja na maelezo yenye kutia moyo kuwa nchi yetu ikipata watumishi wanaoitanguliza nchi, Tanzania inaweza kufuta umaskini. Botswana inategemea almasi kwa mauzo ya nje kwa asilimia 89 ya pato la taifa kwa fedha za ...

Read More »

Odinga anakuwa Rais Kenya

Balile

Na Deodatus Balile, aliyekuwa Mombasa Kuna kila dalili kuwa mwanasiasa Raila Amolo Odinga (73), miaka minne ijayo atachaguliwa kuwa Rais wa Kenya, yaani mwaka 2021. Hivi karibuni nimepata fursa ya kuwa jijini Nairobi na baadaye nikasafiri hadi Mombasa, ambako nimepata fursa ya kukaa na watu wa kada mbalimbali wanaozifahamu siasa za Kenya. Sitanii, katika nyakati tofauti watu niliozungumza nao hitimisho ...

Read More »

Rais Korea Kusini afungwa kwa rushwa

Seoul, Korea Kusini Rais mstaafu wa Korea Kusini, Lee Myung-bak, amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela pamoja na faini ya dola za Marekani milioni 11.5 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 25) kutokana na kukutwa na hatia ya makosa kadhaa ya rushwa. Rais Lee alihukumiwa katika Mahakama ya Seoul wiki iliyopita kwa tuhuma za rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ...

Read More »

Korosho bado ni ‘umiza kichwa’! (4)

Sehemu iliyopita, nilianza kuandika rejea ya makala niliyoiandika miaka 17 iliyopita. Nilisema kule India nako lile shirika la “Cashew Corporation of India” lililonunua korosho zetu zote lilishavunjwa. Hivyo wanunuzi binafsi walikuwa wanajinunulia korosho kiholela kwa viwanda vyao vya kubangulia korosho. Wakati wa vurugu za namna hii serikali yetu ikaruhusu soko huria kwa korosho! Matajiri wale wa India wakawatumia mawakala wale ...

Read More »

Dk. Bashiru utachukiwa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, ametoa kauli ya kijasiri kuhusu ushindi wa chama hicho, akitoa mfano wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ambao ni asilimia 42 pekee ya waliojiandikisha kupiga kura ndio waliojitokeza. Nampongeza kwa dhati Komredi Bashiru kwa kuisimamia imani ile ya Mwana CCM ya “Nitasema Kweli Daima, Fitina Kwangu Mwiko.” Nampongeza kwa sababu ...

Read More »

Tutetea urithi wa lugha zetu

Miezi kadhaa iliyopita nilimsikia jirani yangu Mkurya akitoa somo la nyota kwa wageni Wafaransa. Alitaja tafsiri, kwa Kikurya, ya nyota, mwezi, jua, na hata ya sayari Zuhura. Lugha mama yangu ni Kiswahili, siyo Kizanaki, kwa hiyo hufurahia sana kusikia Mtanzania, tena kijana, akiwa na uwezo mzuri wa kuzungumza lugha yake asilia. Iilikuwa kielelezo cha uwepo wa urithi mkubwa wa tamaduni ...

Read More »

Naomba Mhandisi Mjungi akumbukwe

Na Angalieni Mpendu Rais Dk. John Pombe Magufuli nimekusikiliza kwa utulivu, nimekusoma kwa umakini na nimekuelewa kwa undani katika hotuba yako ya uzinduzi wa Daraja la Mfugale (Mfugale Flyover), eneo la TAZARA, katika makutano ya Barabara ya Mandela na Barabara ya Nyerere wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Kati ya mambo niliyoyaelewa moja wapo ni ‘gharama ya kuwa mwaminifu katika ...

Read More »

Yah: Mheshimiwa Charles Tizeba umetusahau wakulima wako

Ninajua kuwa hautanielewa nikisema umenisahau kwa sababu haujapata nafasi ya kuja kunitembelea hapa kwangu na kuona jinsi ambavyo fuko la alizeti lilivyogeuka kuwa mto wa kulazia kichwa changu huku nikiwaza rundo la mahindi nitaliuza wapi, najiuliza, mihogo niliyonayo niwakabidhi nguruwe au nigawe kwa wagonjwa? Mheshimiwa Waziri, nimehemewa mawazo kwa sababu najua haujui ni kiasi gani sisi wakulima tunaumizwa na mzigo ...

Read More »

Mourinho, mwisho wa enzi!

NA MWANDISHI WETU Alexis Sanchez anaweza kuwa ameokoa kibarua cha Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, kufukuzwa mapema wiki hii baada ya kuwafunga Newcastle United 3-2 mwishoni mwa wiki. Endapo Jose Mourinho ‘The Special One’ atafungashiwa virago, Meneja wa Tottenham, raia wa Argentina, Mauricio Pochettino, anatajwa kurithi mikoba yake. Mourinho amekalia kuti kavu kutokana na timu yake ya Man United kutofanya ...

Read More »

SAM MANGWANA Mwanamuziki asiyechuja

NA MOSHY KIYUNGI Jina la Sam Mangwana si geni masikioni mwa wapenzi wa muziki wa dansi Afrika Mashariki na Kati. Ni mwanamuziki mwenye vipaji vya utungaji na kuimba nyimbo za muziki wa dansi akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mangwana alizaliwa Februari 21, 1945 katika mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wazazi wake walikuwa wahamiaji ambapo baba yake ...

Read More »

Kwako Waziri wa Mambo ya Ndani

Mheshimiwa Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sisi askari wastaafu wa Jeshi la Polisi tunakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ingawa kuna changamoto za hapa na pale. Tunakutia moyo na tunaomba Mungu akuzidishie hekima katika utendaji wako. Ndugu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kubwa. Inaundwa na Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la ...

Read More »

Mtoto wa rais akamatwa na mali za bilioni 36

Sao Paulo, Brazil Vyombo vya usalama nchini Brazil vimekamata fedha taslimu na mali za kifahari za mtoto wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema, vyote vikiwa na thamani ya dola milioni 16 (Sh bilioni 36). Miongoni mwa vito vya thamani vilivyokamatwa ni saa zilizokuwa kwenye mabegi ya msafara wa mtoto huyo. Teodoro Obiang, ambaye ni Makamu wa Rais wa ...

Read More »

Uamuzi wa Canada dhidi ya Kyi ni sahihi

Kama hujamsikia Aung San Suu Kyi, fungua macho upate somo la unafiki mkubwa unaotawala ulimwengu wetu enzi hizi. Su Kyi ni kiongozi wa Myanmar mwenye wadhifa unaofanana na wa waziri mkuu ambaye ni maarufu kama mwanaharakati aliyepinga utawala wa kijeshi wa nchi yake kwa miongo kadhaa na kusababisha kutumikia kifungo cha nyumbani kwa karibia miaka 20 hadi kufikia mwaka 2010. ...

Read More »

Korosho bado ni ‘umiza kichwa’! (3)

Wakati wakulima wa korosho wanaanza kufaidi – (kwa Kimwela ‘kupoka’) neema za korosho, mara mwaka ule wa 1973 serikali ikavunja ile bodi ya mazao, lakini ikaunda mamlaka maalumu kwa zao letu la korosho. Mamlaka hiyo ilijulikana kama CATA (Cashew Authority of Tanzania). Majukumu ya mamlaka hii yalikuwa kuweka bei za korosho, kununua na kuuza korosho. CATA ilishughulikia kikamilifu zao la ...

Read More »

TFF inazibeba Simba, Yanga

Mfumo wa sasa wa ufadhili wa ligi hauna tija kwa taifa, kwani tunaendelea kuzifadhili Simba na Yanga ambazo kitaifa hazina uwezo, wameshuka kisoka ndiyo maana hawashindi. Turudishe mfumo wa Sunlight au Taifa Cup kupata wachezaji wazalendo kutoka vijijini na wilayani. Msomaji wa JAMHURI, Pangani, 0716612960 Lindi hatuna DC Kutokuwa na mkuu wa wilaya Lindi Vijijini kunawanyima uhuru wananchi kuamua mambo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons