Uchumi

Mafanikio Yoyote Yana Sababu (9)

Na Padre Dk Faustin Kamugisha   Nia ni sababu ya mafanikio. Penye nia pana njia. Mtazamo wa “lazima nifanye kitu,” unatatua matatizo mengi kuliko mtazamo wa “kitu fulani lazima kifanyike.” Mtazamo wa kwanza una nguvu ya nia. “Nia yetu inaumba uhalisia wetu,” aliandika Wayner Dyer katika kitabu chake The Power of Intention. Yote ambayo umeyafanya kuna wakati uliyanuia. Mambo mengi ...

Read More »

Benedict Rasha Ndiye Aliyegundua Kuungua kwa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka

Na Albano Midelo Benedict Mapunda (Rasha) mwenye umri wa miaka 66 mkazi wa kijiji cha Ntunduwaro ndiye aliyegundua kuungua moto kwa mgodi wa madini ya makaa ya mawe Ngaka uliopo Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 2006. Inakadiriwa moto huo uliowaka kwenye mgodi huo mwaka 2006 uliteketeza tani milioni sita za makaa ya mawe ndizo.Inaaminika Moto huo ulianza kuwaka ...

Read More »

Matumizi ya Gypsum Kwenye Ujenzi Yanazua Hofu

Mwaka 2011 nililala kwenye hoteli ya mjini Moshi, chumba kilirembwa na dari iliyonakshiwa kwa jasi inayojulikana zaidi kama gypsum. Ilikuwa ni jasi iliyokaa muda mrefu na ilikuwa inapukutika kwa urahisi. Siku iliyofuata niliiugua, nikapatwa na homa kidogo na mafua, ingawa hali hiyo mbaya haikuendelea kwa siku nyingi. Niliamini kwa uhakika kabisa wakati huo kuwa ni kuvuta kwa hewa iliyoathiriwa na ...

Read More »

MKAA MBADALA UNAVYOCHOCHEA HIFADHI YA MAZINGIRA KILIMANJARO

NA JAMES LANKA, MOSHI Ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya kuni na kuchoma mkaa unaotumika na wananchi wengi hasa wa kipato cha chini na cha kati kuwa nishati ya kupikia, unachochea uharibifu wa mazingira katika Mkoa wa Kilimanjaro. Ingawa ni hivyo, ukataji miti huo unatajwa kuwa chanzo cha mapato kwa wananchi wanaowekeza katika biashara ya nishati hiyo mkoani humo. ...

Read More »

GMOS: KIGINGI KWA UFANISI WA KILIMO MANYARA

NA RESTITUTA FISSOO, MANYARA Ni ukweli usiopingika kuwa ili kufikia azma ya Serikali ya kufanya kilimo kuwa biashara, kukuza kipato, matumizi ya sayansi na teknolojia vinahitajika ili kuongeza uzalishaji na tija kwa mkulima. Hata hivyo, teknolojia mpya ya kubadilisha vinasaba vya mimea (GMOs) imeleta hofu kwa wakulima hususani mkoani Manyara kiasi cha kuibua hitaji kwa Serikali kuingilia kati. Hali hiyo ...

Read More »

Rushwa ni Wizi, Dawa Yake ni Uwazi

“Rushwa ni wizi wa fedha za umma”. Hivyo ndivyo Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, Roeland van de Geer, anavyotaka Watanzania waielewe rushwa. Rushwa, kwa mujibu wa Balozi Geer, ni chanzo kikubwa cha ukiukwaji wa haki za binadamu, kushamiri kwa umaskini pamoja na ukosefu wa maendeleo hasa kwenye maeneo ya Serikali za Mitaa ...

Read More »

Ukikata Tamaa, Palilia Matumaini

Usikate tamaa, jua linapozama, nyota na mwezi vinachomoza, kuwa na matumaini. Alexander the Great alipokuwa anafanya kampeni aligawa zawadi mbalimbali kwa rafiki zake. Katika ukarimu wake karibu alitoa kila kitu alichokuwa nacho. Rafiki yake alimwambia: “Bwana hutabaki na kitu chochote.” Alexander the Great alijibu: “Nimebaki na kitu. Nimebaki na matumaini.” Ukibaki na matumaini umebaki na jambo kubwa. “Usimnyanganye mtu fulani ...

Read More »

Ushauri Wangu kwa Dk. Kigwangalla

Kwenye vitabu vya dini tumezuiwa kujisifu, lakini hatukatazwi kutangaza mafanikio. Ndiyo maana nakiri kuwa miongoni mwa wadau tuliosimama imara kuhakikisha tunaondoa ukiritimba wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA), kutoka kwenye mizengwe ili kiwe na manufaa kwa Watanzania na kwa Taifa letu kwa jumla. Kuna wakati mwekezaji mmoja raia wa kigeni alikuwa akimiliki vitalu ambavyo ...

Read More »

Uzalendo si Suala la Hiari

Desemba 8, mwaka huu, Taifa letu lilizindua kampeni ya Uzalendo hapa nchini. Uzinduzi ule ulifanyika Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na ulifanywa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Magufuli. Hili ni jambo zuri na muhimu sana kwa Taifa kujitambua na kuwaandaa watoto, kizazi kipya wasipotoshwe na tamaduni za kigeni zinazoonekana katika ma-runinga. Mwaka ...

Read More »

Ndugu Rais, Maisha Yangu na Baada ya Miaka 50

Ndugu Rais, waaminio katika juzuu wanasema chapisha au potea. Najua iko siku sitakuwapo katika ulimwengu huu wa mateso kwa sababu sote tunapita tu hapa duniani. Sijui Mwenyezi Mungu ametupangia siku ngapi za kuishi, mimi na wengine. Lakini tuzikumbuke siku za ujana wetu ili tumtukuze Mungu. Ndugu Rais, Mwenyezi Mungu ametuumba na masikio mawili lakini mdomo mmoja tu, makusudio yake ilikuwa ...

Read More »

Wachina Waamua Kujitosa Muhogo Tanzania

Balile

Leo naomba kuanza makala yangu kwa kukutakia heri ya Krismasi mpendwa msomaji wangu. Lakini pia nichukue fursa hii kuwashukuru nyote mlioniletea salaam za pole kwa wiki yote iliyopita wakati nimelazwa na kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam. Kipekee niwashukuru Dk. Juma na Dk. Victor Sensa wa Muhimbili kwa vipimo na tiba walizonipatia hadi sasa naandika makala ...

Read More »

MWALIMU NYERERE: MAENDELEO NI KAZI

Hotuba ya Rais wa Chama, Mwalimu Julius K. Nyerere, Kwenye Mkutano Mkuu wa TANU wa 16. Waheshimiwa sasa ningependa kuufungua Mkutano wetu rasmi. Nasema katika ufunguzi huu kazi yangu kwa leo itakuwa, asubuhi hii, ni kuwasilisha kwenu Taarifa ya mambo yaliyofanyika, katika utekelezaji wa maazimio tuliyoyapitisha katika mkutano uliopita. Hiyo ndiyo kazi nitakayoifanya. Kabla ya kuifanya kazi hiyo, ningependa kueleza ...

Read More »

Turejeshe Rasilimali za Umma Pasipo Migogoro

Tangu ilipoingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015, Serikali ya Rais John Magufuli imefanya uamuzi mgumu unaohusu kurejesha mali za umma zinazodaiwa kuhujumiwa pasipo kujali maslahi mapana ya nchi. Ipo orodha ndefu ya matukio yanayodhihirisha kufikiwa kwa hatua hiyo, ingawa kwa upande mwingine pamekuwapo wakosoaji wa mbinu na njia zinazotumika katika utekelezaji wake. Pamoja na changamoto zinazosababisha ...

Read More »

Njaa isitufikishe huko

Kwa sisi tuliozaliwa na kukulia vijijini miezi ya Agosti, Septemba, Oktoba, Novemba na Desemba huwa ni miezi ya sherehe, harusi, ngoma za kila aina na hata ndugu kukumbukana (okuzilima). Miezi hii huwa watu wana furaha. Kingazi cha Julai kinakuwa kimekwisha na hata mavuno waliyopata mwezi Machi, inawabidi washindane kuyamaliza ghalani maana Septemba na Oktoba ni miezi ya mavuno. Mahindi kwa ...

Read More »

Ujenzi wa Uzalendo si Suala la Mjadala

Wale wanaosikiliza hotuba za Rais John Magufuli, kuna kitu wanakipata mara kwa mara. Sijasikia hotuba yake yoyote akikosa kutaja neno ‘uzalendo’. Amediriki kusema viongozi, akiwamo yeye, watapita lakini Tanzania itabaki; na ili ibaki, Watanzania wote hatuna budi kuwa wazalendo. Rais anaamini kuwa kwa kujenga uzalendo, Tanzania itakuwa na nguzo imara za kuifanya iwepo leo na hata kesho. Kwa wale wanaosikiliza ...

Read More »

Mafanikio Yoyote Yana Sababu (2)

Kufikiria vizuri ni sababu ya mafanikio. Tazama mbele ufikiri. Papa Fransisko alisema kuna lugha tatu: ya kwanza fikiria vizuri, ya pili hisi vizuri, ya tatu tenda vizuri.  Kufikiria vizuri ni msingi wa mafanikio. Kuna aina mbalimbali za kufikiri. Kwanza ni kufikiria kwa ‘kufokasi’. Fokasi ni mahali miale ya nuru ikutanapo. Kuwa makini na lengo lako. Mambo ambayo si muhimu yanayokuondoa ...

Read More »

Mfuko wa Jimbo ni ukiukaji Katiba

Moja ya hukumu murua kabisa kutolewa na mahakama ya juu kabisa nchini Kenya hivi karibuni, inahusu Mfuko wa Jimbo kwa kutamka pasipo kumung’unya maneno kuwa ni haramu kwa mbunge kugeuka mtendaji wa fedha za umma. Majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Kenya wametamka kuwa Sheria ya Mfuko wa Jimbo (Constituency Development Fund Act), ya mwaka 2003 inakiuka Katiba ya nchi ...

Read More »

Maandiko ya Mwalimu Sehemu Maendeleo ni Kazi

Lakini kulipa ni jambo la lazima kabisa, hakuna kusema kwamba atapata madawa ya bure, madawa ya bure yanatoka wapi? Hatuwezi tukasali misikitini na makanisani, tukamwambia , Mwenyezi Mungu, eee, tuletee kwinini, hawezi kuleta kwinini. Sasa hilo ndilo jambo moja ninalitilia mkazo katika taarifa hii kwamba kabla ya kuanza kusema tumefika kiasi gani cha elimu yenye manufaa. Lazima ujue tumeongeza uwezo ...

Read More »

Tujenge Uzalendo Kupitia Uchumi

Wiki iliyopita nchi yetu imesherehekea miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara). Wakati tunapambana kupata uhuru, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeongoza harakati hizo, alisema nchi yetu ilikuwa inapambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini. Na alisema ili nchi ipate mafanikio inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Ukipima kigezo cha siasa za kufanya uchaguzi, naamini Tanzania tunapasi. ...

Read More »

Asante Sana Waziri Mkuu, Uhifadhi Umeshinda

Desemba 6, 2017 itabaki kuwa siku muhimu katika kumbukumbu za kazi nilizopata kuzifanya. Hii ni siku ambayo Serikali, kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ilitangaza ‘kuumaliza’ mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo. Naikumbuka siku hii, si kwa sababu ya kumalizwa kwa mgogoro, bali kwa sababu Serikali imethubutu kutenda kile ambacho Serikali mbili au tatu zilizopita zilifeli. Wala sitoikumbuka siku hii kama ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu x (1)

Wanatoka tumbo moja lakini hawafanani. Ni methali ya Tanzania. Watoto wenye wazazi walewale, walionyonya titi lile, na kusoma shule ile ile kimafanikio wanatofautiana. Kinachowatofautisha ni sababu x. Wanadarasa wakiwa na viwango tofauti vya ufaulu darasani. Inatokea aliyetangulia darasani hapati mafanikio katika maisha kuzidi aliyekuwa wa kumi. Tofauti ni sababu x. Sababu x ni siri ya mafanikio. Watu wanatoka chuo kimoja wamefundishwa ...

Read More »

Nani Wanaoratibu Biashara ya ‘Kubeti’?

Mpita Njia (MN) ni miongoni mwa wale wanaoamini kuwa utandawazi maana yake si kuachia kila kitu kijiendeshe kienyeji. Anajiuliza, mbona huko ulikozaliwa huo utandawazi kuna mambo mengi yamepigwa kufuli? Mbona huku kwetu kila jambo – lililo baya au lililo jema- linaachiwa tu? MN amefikia hatua hiyo baada ya kuona hizi nyumba zenye kuendesha michezo ya ‘kubeti’ zinavyoongezeka. Anashangaa kuona Serikali ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons