Bei ya mafuta duniani imepungua kwa kiasi kikubwa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili.
Mapema Jumanne, pipa moja la mafuta uliouzwa kwenye masoko ya kimataifa ulikuwa na thamani ya dola 103.42, huku mafuta ya Marekani yakiwa karibu na dola 103.25 kwa pipa. Hata hivyo, bei bado iko juu kuliko kipindi cha kabla ya mzozo kuanza Februari 28.
Mtaalamu wa uchumi wa nishati kutoka Japan, Ichiro Kutani, alisema kushuka kwa ghafla kwa bei kunahusiana moja kwa moja na tangazo la Trump. Hata hivyo, bei haiwezi kurudi katika kiwango chake cha awali cha takribani dola 70 kwa pipa kwa sababu ya uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati.
Wakati huo huo, masoko ya hisa barani Asia yamepanda: Nikkei 225 ya Japan imeongezeka kwa takribani 4% na ASX 200 ya Australia kwa karibu asilimia 3.

