*Dar es Salaam yaongoza kitaifa kwa maambukizi,
*Ujazo abiria kwenye daladala, msongamano wa makazi wachangia
Na Kulwa Karedia, JahuriMedia, Dar es Salaam
KWA miaka kadhaa iliyopita, ugonjwa wa kifua kikuu (TB), ulikuwa unatibika kwa mwaka mzima, sasa mambo yamebadilika ambapo mgonjwa anayetumia vizuri dawa anapona ndani ya miezi sita tu,JAMHURI linaripoti.
Hatua hiyo inatokana na juhudi kubwa zilizofanywa na serikali ili kukabiliana na ugonjwa huo ambao unaonekana kushamiri zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na asilimia 17 kitaifa, unatibika kwa idadi ndogo ya vidonge tofauti na miaka ya nyuma.
Mtaribu wa Kifua Kikuu na Ukoma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyala jijini Dar es Salaam, ,Dk Saudan Masawe amesema ugonjwa huo unatibika kwa idadi chache ya dawa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwa mingi.
“Ugonjwa huu unatibika vizuri kabisa kwa idadi chache ya dawa tofauti na miaka ya nyuma, hivi sasa mgonjwa anaweza kutumia vidonge vichache ndani ya miezi sita na kupona,”amesema
Amesema hatua hiyo inatokana na na serikali kupambana na kuongeza juhudi kwa kushirikiana na mashirika ya nje pamoja na taasisi mbalimbali za tafiti, zimeweza ku[punguza hadi kufikia miezi sita ya matibabu na matumizi ya vidonge vine tu kwa matumizi ya mtu mwenye uzito wa kilo 50 ambavyo vinachukuliwa kama idadi kubwa.
“Miaka ya nyuma mtuli akiugua kifua kikuu kwa mara ya kwanza, alikuwa anatumia dawa nyingi pamoja na sindano ilikuwa inachukuwa muda mrefu, lakini kutokana na serikali kupambana kwa kushirikiana na mashirika ya nje na pamoja na taasisi mbalimbali za tafiti, zimeweza ku[punguza kufikia miezi sita ya matibabu.
Amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu kujitokeza kutokana na kuelemika na kuwa wawazi na wengi wao wamekuwa wakipata elimu ya ugonjwa huo.
“Mtu anapokuja kutibiwa hospitalini kwa madaktari katika vitengo vya kaiwada yeye mwenyewe anakuwa chanzo cha kukumbusha kupima ugonjwa huu kwa sababu anatambua ni ugonjwa ambao unaambukiza vipi, pengine labda alishawahi kuishi na mgonjwa wa aina hiyo.
“Sasa hivi imekuwa kila mtu ana anauelewa maana ilikuwa kama TB kama kitengo maalumu ambacho kina watalaamu wake, sasa hivi kila mtaalamu wa afya anaweza kusaidia kwa sababu ni kitu ambazo kimezungumzwa sana na elimu yake imekuwa ikitolewa muda mrefu, kila mmoja amepata uwelewa, ikitokea mtu amefika na kuonana na daktari aliyetoka kitengo kingine ni rahisi kugundua hizi ni dalili zinazonyemelea kuwa na kifua kikuu.

Amesema Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kitaifa kwa kuwa na wagonjwa wengi ambao kitaifa wanafikia asilimia 17 tofauti na mikoa mingine.
“Mkoa huu una watu wengi sana ni mkoa ambao ambao unachangia asilimia 17 ya ugunduzi wa kifua kikuu kutokana na kuwapo mwingiliano mkubwa watu, shughuli mbalimbali na shughuli za viwanda.
Amesea kutokana na hali hiyo, imeilazimu serikali katika wilaya za kisekali zimefanywa kama mikoa kitibii ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo sasa linakabiliwa kisawasawa.
“Ukija Temeke, Ilala Kigamboni, Kinondoni pamoja na Ubungo. Sasa katika yote hii kwa Dar es Salaam Mkoa wa Temeke ndiyo unaongoza ugonjwa, ukifuatiwa na Ilala, Kigamboni kisha Kionondoni,”amesema.
Alipoulizwa kwanini Temeke inaongoza, mtaalamu huyo wa afya amesema “Temeke ni eneo ambalo lina watu wengi sana, hata ukiangalia aina ya usafiri, magari ya Mbagala yanajaza sana watu, angalia makazi yalivyobanana na msongamano mkubwa.
Amesema wagonjwa TB kwa Tanzania nzima unafikia 128,000 mpaka 137,000 kwa mwaka, huku Mkoa wa Dar es Salaam ukadiriwa kuwa una wagonjwa 20,000 kwa mwaka, huku Mkoa wa Temeke una wagonjwa 5,055 kwa takwimu za mwaka 2023, huku maambuziki yakiwa 338/100,000 wakati kiwango cha maambukizi kwa Kinondoni ni watu 259/100,000.
“Ukija maeneo ya Ilala kama Gongolamboto, Chanika hivyo ukiangalia vyombo vya usafiri watu wengi wanakuwa na msongamano unaochangia tatizo hili, ni maeneo ambayo yanapatikana magereza, machimbo,”amesema.
Kutokana na hali hiyo, amesema katika mambo ambayo serikali imefanya ili kuwasaidia wakazi wa mikoa hiyo ni kuongeza usimamizi wa karibu na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi.
“Hawa watu wanatoka katika jamii, serikali imefanikiwa kutenga “watu wa afya jamii” yaani wasaidizi wetu, tunawapa utalaamu wa ugonjwa huu kwa sababu wengine ambao waliwahi kuugua tunachukuwa wale ambao wanakuwa na sauti ya kusikilizwa katika jamii. Kwa mfano waganga wa kienyeji , wauza dawa za asili tumekuwa nao katika kampeni zetu za ugonjwa huu.
“Anapokuwa anamuuzia mtu dawa ya kikohozi mara mbili au mara tatu, hivyo tunaoata watu kupitia njia hii, pia kwenye jamii wapo watu wanapenda kujitolea au waliwahi kuugua kifua kikuu wakapona, lakini wana ushawishi wa kuongea na watu wengine wanafanya waje kupima. Tukigundua watu kama hawa tunawaingiza kwenye taasisi zetu tunakuwa tunasaidiana nao kuibua tatizo hili.
“Kumbuka kuna wale watu ambao wanajindunga wanakuwa na masikani zao, tunapopata mtu wa kwao ambaye wanaelewana ama anajidunga au aliwahi kujidunga inakuwa rahisi kwetu, tunamwelemisha kuhusu ugonjwa huu akielewa anakuwa kama mwalimu kwao maana mwisho wa siku anachukuwa makohozi anatuletea tunayapima na kugundua wagonjwa wapya,”amesema.
Alipoulizwa namna ya nzuri ya kukabiliana na kufikisha kirahisi ujumbe kwa jamii, Dk Saudan amesema serikali imechukuwa hatua mbalimbali zikiwamo za kueleka ujumbe mfupi wa maneno (SMS).
“Utaratibu huu ulikuwepo ssema ni vile haujaenea kwa watu wengi,pia serikali ilianzisha mfumo wa Tambua TB APP, hii tulikuwa tunaelekeza watu na mabango yalikuwepo, sijui kwa mikoa mingine lakini kwa Dar es Salaam watu wengi wameelewa. Mfumo huu mtu anatumia simu yake tena bila bando au gharama yoyote,”amesema.
Amesema mikoa 10 inayoongoza kwa ugonjwa huo, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mbeya, Arusha,Kagera,Shinyanga, Kilimanjaro ambako wagonjwa hugundulika mapema zaidi kutokana na uwepo wa hospitali ya kitaifa ya Kibong’oto.

