Iran imeonya jana kuwa itajibu kwa mashambulizi makali na ya muda mrefu dhidi ya majeshi ya Marekani iwapo Washington itaanzisha tena mashambulizi.
Tehran pia imesisitiza kuwa inaendelea kudhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz, hali inayotia doa mipango ya Marekani ya kuunda muungano wa kimataifa wa kufungua tena njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta.
Miezi miwili tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, njia hiyo muhimu ya baharini bado imefungwa, hali inayokatiza karibu asilimia 20 ya usambazaji wa mafuta na gesi duniani. Hatua hiyo imepelekea kupanda kwa kasi kwa bei za nishati duniani na kuongeza hofu kuhusu hatari ya kudorora kwa uchumi wa dunia.
Na huko mjini Tehran, mifumo ya ulinzi wa angani imesikika usiku wa kuamkia leo, huku mashirika ya habari ya nchi hiyo ya Tasnim na Fars yakiripoti kuwa mifumo hiyo ilianzishwa ili kukabiliana na ndege ndogo na droni za kijasusi bila kutoa maelezo zaidi.



