Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea kupeleleza kwa uzito mkubwa tukio la mauaji ya ya mtu aliyetambulika kwa jina la James Rogers Temba mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha IFM Dar es Salaam ambaye mwili wake ulikutwa unaelea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka katika mto Msimbazi eneo la Kipawa Ilala tarehe 30.4.2026 huku ukiwa hauna kichwa.
Polisi Dar es Salaam imewakamata watuhumiwa wanne ambao ni 1.Steven Rogers Chaka, Mmbugu miaka 31, Afisa maabara Mkazi wa Bomang’ombe Hai Kilimanjaro 2. Anna Frank Lema @happines, Mchaga, miaka 30, mfanyabiashara Mkazi wa Tabata Chang’ombe 3. Twalibu Khamis @mputo miaka 23 mkazi wa Kigogo Kati 4. Michael John @tambali miaka 26 mkazi wa Kigogo Kati.
Vipo pia baadhi ya vielelezo ambavyo vinachunguzwa kuhusiana na tukio hilo.Wito wa Jeshi la Polisi kwa wananhi ni kuwa watulivu ili kila aliyehusika kulingana na ushahidi aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.


