Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kupiga Vita UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND), Andrew Hammond ofisini kwake jijini Dodoma.

Dkt.Jingu amesema mazungumzo hayo yalilenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya afya katika maeneo yao.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu akifanya mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka (GLOBAL FUND), Andrew Hammond ofisini kwake Jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na mfuko huo kwani umekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vifaa tiba kama ilivyo azima ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga miundombinu na kuboresha masuala ya tiba kwa wananchi.

Naye Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND),Andrew Hammond ameishukuru Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko huo katika kupiga vita maradhi ya Kifua Kikuu, Malaria na Ukimwi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Kaspar Mmuya akifuatilia kikao.

Ameahidi kuwa Mfuko wa Dunia utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na magonjwa hayo hapa nchini kwa kuelekeza rasilimali fedha kwa ajili ya kununua dawa pamoja na kuboresha mifumo ya utoaji huduma ya afya.

Meneja Mkaguzi kutoka  Ofisi kuu ya Ukaguzi ya Mfuko wa Kimataifa wa Kupiga Vita UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND) . Andrew Hammond akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

By Jamhuri