Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam

MWENGE wa Uhuru umezindua miradi saba ya maendeleo Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya shilingi bilioni 17.

Akizungumza mara baada kuzindua miradi hiyo ya maendeleo mkuu wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda alisema katika miradi hiyo iliyozindiwa na kiongozi wa Mbio za MWENGE kitaifa Isimail Ally Ussi alisema baadhi ya miradi hiyo mradi wa ujenzi wa barabara Masaki jiwe la msingi ,Kituo cha Polisi Tuangoma,mradi wa shule ya sekondari Magaya ,

Aidha mkuu wa Wilaya ya Mapunda ,alitaja miradi mingine kuwa ni kituo cha vijana mabegi House, mradi wa hospitali ya Wilaya jiwe la msingi ,shule ya sekondari Yombo ,Vituka na uzinduzi wa mradi wa wapinga rushwa ikiwemo taarifa ya lishe kukagua shughuli za lishe.

“Manispaa yetu leo imezindua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 17 fedha za maendeleo za mapato ya ndani tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta pesa nyingi za miradi ya maendeleo Manispaa yetu “alisema Mapunda.

Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Mbagala Abdalah Chaurembo alisema wanamshukuru Rais kwa kutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo wamejenga kituo cha Polisi cha Tuangoma kituo daraja C lakini kitapewa daraja D kitakuwa kinajitegemea .

Mbunge Chaurembo alisema Rais amefanya makubwa mwezi Oktoba yeye na wananchi wake watamlipa kwa kupiga kura nyingi.

“Jimbo la Mbagala limezaa jimbo jipya la Chamazi Mkoa Dar es Salaam kwa sasa maendeleo yote Serikali wataelekeza jimbo jipya la chamazi nawaomba wananchi muwe na imani ya ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ” alisema Chaurembo.

Kiongozi wa nbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Isimail Ally Ussi, alipongeza Manispaa ya Temeke kwa kufanya kazi nyuri katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani ambapo alisema mwenge wa uhuru umeleta heshima kubwa Tuangoma ,Tuangoma imekuwa kiuchumi hivyo Manispaa imelazimika kujijenga.

Mwenge wa Uhuru umetokea Mkoa wa Lindi umewasili Mkoa Dar es Salaam kuzindua miradi ya maendeleo kuanzia Juni Mosi mpaka Juni tano kabla kukabidhiwa Mkoa Tanga,mkuu wa mkoa Albert John Chalamila, alipokea kutoka kwa mkuu wa mkoa Lindi Zainab Terack .

Mkuu wa Mkoa Chalamila alipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa Lindi na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Temeke ,Sixtus Mapunda ,

Awali Mkuu wa Mkoa Albert John Chalamila alisema mwenge wa uhuru utazindua miradi 37 ya mkoa huo na kauli mbiu Jitokeze Kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na utulivu.