Watu watatu wamefariki na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Maonyoni mkoani Singida

katika Kijiji cha Kitopeni Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida, huku mmoja akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Gaspar Itigi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Stella Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kamanda amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Novemba 27, 2022 ikihusisha gari ndogo aina ya Mazda na lori.

“Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu wawili papo hapo na mmoja alifariki wakati anapatiwa matibabu,” amesema.

Kamanda amesema kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alihama kabisa upande wake na kulifuata gari dogo na kusababisha ajali hiyo.