Wafungwa kadhaa wakiwemo askari magereza wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo Novemba 8, 2022 katika eneo la Kaloleni wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,Mbaraka Batenga amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa, chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

Amesema, gari hilo lilikuwa linatoka kambini kwenda katika shughuli za kila siku za kawaida.

By Jamhuri