Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yamejikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, afya, elimu na nishati.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan katika Ofisi
Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi Shelukindo amemhakikishia Katibu Mkuu huyo ushirikiano wa dhati katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na na Indonesia. Aidha,  amemueleza kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni mazuri na salama na kuwasihi wawekezaji kutoka Indonesia kuchangamkia fursa zilizopo.

Naye, Bw. Herawan amepongeza uhusiano imara uliopo baina ya serikali hizi mbili (Tanzania na Indonesia) na kuongeza kuwa Indonesia itaendelea kushirikina na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya nchi zote mbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep
Herawan (aliyevaa miwani kushoto) akizungumza wakati wa kikao chake
na mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Ofisi Ndogo
za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (katikati kulia) akimsikilza
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep
Herawan wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Mazungumza baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep
Herawan yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

By Jamhuri