Na Abel Paul,Jeshi la Polisi -Arusha

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha limefanya operesheni maalum iliyolenga kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa mabasi ambayo yatoa huduma Mkoani humo huku likimkamata dereva Sostenes Mgaya (42) Mkazi wa Arusha kwa kosa la kujaza abiria kupita kiasi.

Katika Operesheni operesheni hiyo iliyongozwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Alijua Samutt amesema operesheni hiyo imebaini basi la Kampuni ya Struggle line ambalo amesema limezidisha abiria 33 ambapo amesema kitendo hicho ni kinyume na sheria za Usalama Barabarani huku akibainisha kuwa inahatarisha maisha ya abiria.

ASP Alijua amesema dereva wa basi hilo ameonywa kwa kupigwa faini kwa kosa hilo huku akibainisha kuwa endapo dereva huyo atakamatwa tena kwa kosa hilo ataadhibiwa kwa kufungiwa leseni yake.

Aidha ametoa wito kwa madereva wengine wenye tabia ya kuzidisha abiria kuwa kikosi hicho akitomwonea muhari dereva atakaye bainika kuja abiria kupita kiasi cha uwezo wa gari husika.