Mwanamke anayedaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili anayefahamika kwa jina Grace Kihumba(30) mkazi wa Wang’ing’ombe mkoani Njombe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumshambulia baba yake mdogo Tiles Kihumbu (60) akiwa usingizini na kisha kuzikata sehemu za siri na kuziondoa.

AkIfanyiwa mahojiano baada ya kukamatwa na maofisa wa jeshi la polisi mwanamke huyo amesema amefanya hivyo kutokana na kukasirishwa na kitendo cha wanafamilia kuendelea kusherekea wakati yeye anaendelea kuumwa licha ya kutoa hela za matibabu kwa mzee huyo ambaye anadaiwa kuwa ni mtaalamu wa tiba asilia.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ameeleza kuwa mwanamke huyo amefanya kitendo hicho kwa baba yake mdogo aliyekuwa amelala kwenye mkek na akiwa amelewa.

Katika tukio jingine Kamanda Issa amesema jeshi hilo linamshikilia kijana anayefahamika kwa jina la Baraka Alfonce mkazi wa kitongoji cha Kimbila Ludewa mjini kwa tuhuma za kuhusika kumkata kiganja cha mkono bosi wake baada ya kutomlipa fedha kiasi cha elfu 65

By Jamhuri