Dereva wa bodaboda Idrisa Said Bayaga (32) wa kituo cha waendesha pikipiki cha Nyerere Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kushiriki tendo la ndoa na mtoto wake mwenye umri wa 11.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gosper Luoga.

Mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Gregoli Mhangwa, ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe kwa nyakati tofauti kwa kuanzia kipindi cha mwezi Aprili mwaka huu hadi mwezi Septemba .

Aidha hakimu amesema kuwa kitendo hicho ni kutenda kosa kinyume na kifungu cha sheria Namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.

Mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka hayo na mwanasheria wa Serikali alikana na mashtaka hayo.

Jengo la Mahakama ya Hakimu mkazi katavi na Mahakama ya wilaya ya Mpanda

Baada ya mtuhumiwa kukana mashtaka hayo mwendesha mashtaka Gregoli Mhangwa aliiambia Mahakama kuwa upande wa mashtaka umeishakamilisha upelelezi wa kesi hiyo .

Zinazohusiana

– Mchungaji abaka, alawiti, atoroshwa

Ahukumiwa kuchapwa viboko 24 kwa kujaribu kubaka

Hivyo aliiomba Mahakama iweze kuendelea na hatua zinazofuata za kimahakama kufuatia kukamilika kwa upelelezi uliofanywa na pande wa mashtaka .

Kufutia maombi hayo ya upende wa mashitaka Hakimu Luoga alikubaliana na hoja hiyo iliyotolewa mbele yake na upande wa mashitaka ambapo mtuhumiwa Idrisa Said Bayaga alisomewa hoja za awali za mashtaka .

Baada ya kutolewa mahakamani hapo hoja za awali kuwasilishwa Mahakani hapo Hakimu Mkazi mfawidhi Mwandamizi Gosper Luoga aliiambia mhakama kuwa mdhamini wa mshitakiwa upo wazi na anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyo hamishika lakini mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo Desemba 5,2022 itakapoanza kusikilizwa ambapo mtuhumiwa amekwenda rumande.