JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Mengi: Fundisheni watoto kumcha Mungu

Kuwafundisha watoto kumcha Mungu ni dhana nzuri inayowajenga katika maadili ya kuwawezesha kufanikiwa maishani, amesema Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi.

Amefafanua kwamba kumcha Mungu kunamfanya mtoto kuwa mwema, mkweli na mwaminifu, tabia ambazo ni nyenzo muhimu katika kufikia mafanikio ya kiuchumi na kijamii.

“Ni jambo la msingi kwa mzazi kumwandaa mtoto aweze kufanikiwa maishani. Kumfundisha mtoto amweke mbele Mwenyezi Mungu kutamfanya awe mnyenyekevu, mkweli na mwaminifu ili hata akikopa arudishe, maana hakuna anayetaka kufanya biashara na mtu mwongo na anayejivuna,” amesisitiza.

Sakata la Tamisemi lachukua sura mpya

Sakata la Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, kudaiwa kutoa zabuni ya uchapaji wa nyaraka za Serikali kwa Kampuni ya Yuko’s Enterprises Ltd ya mkoani Pwani bila kufuata taratibu limechukua…

JWTZ ngangari

*Wasubiri amri ya Rais Kikwete kwenda Sudan
*Wasema wao wako tayari kulinda maisha ya watu
*UN imewaomba baada ya kuisambaratisha M23
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liko tayari wakati wowote kupeleka vikosi vyake kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Ofisi ya Waziri Mkuu watumbua fedha dawa za kulevya

 

Vita dhidi ya dawa za kulevya inakuwa ngumu baada ya watendaji waliokabidhiwa jukumu la kudhibiti biashara hii haramu kuugeuza mradi, mpango wa kutoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya.

Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini mpango wa kutoa matibabu kwa watu walioathirika na dawa za kulevya unaojulikana kama Medication Assisted Treatment (MAT) uliopaswa kuanza Agosti, mwaka huu tayari umeanza kuhujumiwa.

JWTZ ngangari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liko tayari wakati wowote kupeleka vikosi vyake kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Wahamiaji haramu waivamia Tanzania

*Wakongo, Wanigeria waongoza, wahusishwa wizi wa fedha benki, uuzaji dawa za kulevya

Wimbi la wahamiaji haramu linazidi kuitesa nchi, ambapo sasa raia wa Congo na Nigeria ndio wanaongoza kwa uhalifu huo.

Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, ameithibitishia JAMHURI wiki iliyopita, akisema jitihada zaidi zinahitajika kukabili tatizo hilo.