Category: Maoni ya Mhariri
Kamati Kuu CCM ikomeshe mgogoro unaofukuta Bukoba
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kukutana wiki hii kutafuta ufumbuzi wa mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera. Imeshadhihirika wazi kuwa mgogoro huo ni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Meya Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
Wezi wa fedha za Smart Partnership washitakiwe
Kwa wiki kadhaa gazeti la JAMHURI tumeandika habari za ufisadi wa mamilioni ya shilingi kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue).
Kuna wamachinga wanaovuna mamilioni, walipe kodi stahiki
Hakuna binadamu anayependa kulipa kodi. Lakini Serikali haiwezi kujiendesha bila kodi, hivyo ni wajibu wa kila mtu mwenye sifa za kulipa kodi, kufanya hivyo.
Rais JK, orodha ya mapapa wa mihadarati imeyeyukia wapi?
Katika gazeti hili kuna barua iliyoandikwa na mmoja wa Watanzania walio kwenye magereza Hong Kong, kutokana na usafirishaji mihadarati.
Tanzania inapotea njia
Mwishoni mwa wiki zimetokea habari za kusikitisha. Mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad, amemwagiwa tindikali usoni na sasa amepelekwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.
Matusi kwa Rais wetu hayakubaliki
Kwa muda sasa, kumekuwapo maneno mengi kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda yakimlenga Rais wetu, Jakaya Kikwete. Chanzo cha yote haya ni mapendekezo ya Rais Kikwete ya kumwomba Rais Kagame aketi na waasi wa kundi la FNBL ili kukomesha mapigano na mauaji yanayoendelea Rwanda na upande wa mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).