Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Arusha

Wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi hususan Wakala wa Biashara za Utalii, watoa huduma za malazi, Wakala wa Safari na waongoza watalii wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na Onesho la _Swahili International Tourism Expo (SITE) litakalofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 21 hadi 23, mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana Jijini Arusha alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo la Sita litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

“Fursa hizo ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho, ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali mtajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE” aliongeza Mhe Balozi Dkt. Chana alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo la Sita litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

“ Fursa hizo ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho, ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali mtajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE” aliongeza Balozi Dkt. Chana

By Jamhuri