Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia leo Jumatano, Januari 4, 2023 huku bei ya dizeli ikiendelea kupaa.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato imeonyesha kuwa katika jiji la Dar es Salaam bei ya mafuta ya dizeli itaongezeka hadi Sh,3, 295 mwezi huu ikitokea Sh.3,247 Desemba.

Kwa upade wa mikoa ya Tanga na Mtwara bei ya mafuta ya dizeli imeongezeka kwa Sh.91 na Sh.135 kwa lita mtawalia.

Bei ya mafuta ya petroli imepungua kidogo hadi Sh2,819 mwezi huu kutoka Sh2,827 Desemba jijini Dar es Salaam, huku ongezeko likiwa kubwa kwenye mikoa ya Tanga na Mtwara ambayo itauza mafuta hayo kwa Sh2,993 na Sh2,979 mtawalia.

Mei 2022, Serikali iliweka ruzuku ya Sh100 bilioni kwa ajili ya kupunguza makali ya bei.

By Jamhuri