Takriban watu saba wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya na fisi wilayani Tarime mkoani Mara.

Tukio hilo limetokea mapema leo asubuhi Februari,21 2023 eneo la Bugos nje kidogo ya mji wa Tarime , viongozi wa eneo hilo wamesema.

“Idadi ya majeruhi waliopata matibabu hapa Hospitali ya Tarime ni saba. Hatujui kama watu wengine watakuja,”

kilisema chanzo kilichokataa kutajwa jina lake, katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ambako majeruhi walikimbizwa kwa matibabu.

By Jamhuri