Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni amemsimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero (OCD) Shedracck Kigobanya huku akimuhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC CID), Daud Mshana kwa kushindwa kuwasimamia askari wake na kudaiwa kunyanyasa wananchi na kuwabambikia kesi.

Maamuzi ya Waziri Masauni yamekuja baada ya wananchi waa Ifakara kulalamika katika mkutano wa hadhara kuwa kuna baadhi ya askari Polisi wa Wilaya hiyo ya Kilombero wanatumia nafasi zao vibaya na kunyanyasa Wananchi.

Wananchi hao walisema mara nyingi wawanapokamatwa hufikishwa katika Kituo cha Polisi Ifakara lakini lugha wanazopewa sio za kiuungwana huku wengine wakiwatuhumu kushirikiana na Watu wenye fedha na kuwapokonya haki Wananchi wanyonge.

Baada ya malalakimo hayo Masauni akatoa msimamo wa Serikali ambapo aliswasimamisha kazi na kuwahamisha maofisa hao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotolewa za Wananchi kwa Jeshi la Polisi.

By Jamhuri