Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Oktoba 12, 2023 imemhukumu kifungo cha maisha gerezani, Seleman Mjema (50), mkulima na mkazi wa Mikungani wilayani Arumeru baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Akisoma hukumu hiyo kesi namba 51 ya mwaka 2023 Hakimu wa Mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 11, 2023, saa 07:00 mchana huko katika maeneo ya Mikungani Kata ya Mbuguni wilayani humo kabla ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia.